728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, August 29, 2016

  TaBSA KUWANOWA WACHEZAJI VIJANA WA MPIRA WA MAGONGO

   

  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

  29/08/2016

  Dar es Salaam.
  CHAMA cha mchezo wa magongo nchini (TaBSA) kwa kushirikiaa na wadau wa mchezo huo kutoka Marekani kimeandaa kambi ya mafunzo ya majaribio kwa wachezaji vijana yatakayofanyika Jijini Nairobi Kenya tarehe 2-4 Septemba mwaka huu.

  Kambi hiyo ni sehemu ya maandalizi ya Tanzania kwa ajili ya michezo ya olimpiki ya inayotarajiwa kufanyika mwaka 2020 katika Jiji la Tokyo nchini Japan.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa TaSBA, Bw. Alpherio Nchimbi alisema mafunzo hayo yatawahusisha wanafunzi kutoka shule za Sekondari za Azania, Kibasila, Temeke na Tiger Klub.

  Nchimbi aliwataja wanafunzi 5 waliochaguliwa kuhudhuria mafunzo hayo ni Djeskan Dihonga na Leodgar Leonidas (Azania), Nathan Joram na Peter Pius (Kibasila) na Musa Mbugi (Temeke) na Abdulwahid Anwar kutoka klabu ya Tiger.

  Nchimbi aliwata taratibu za maandalizi za safari hiyo zimeanza ikiwemo kuomba ruhusa kutoka kwa Viongozi wa shule hizo.

  “Endapo kijana atafanya vizuri katika majaribio haya ni nafasi kwake kupata scholarship ya masomo na mafunzo ya mchezo huu nchini Afrika kusini na marekani” alisema Nchimbi.
  MWISHO
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: TaBSA KUWANOWA WACHEZAJI VIJANA WA MPIRA WA MAGONGO Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top