728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, August 3, 2016

  SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAZINDUA VYUMBA VYA MAPUMZIKO VYA KISASA UWANJA WA KIMATAIFA WA LOS ANGELES


  Kutoka kushoto Makamu wa Rais wa Shirika la Ndege la Etihad Kituo cha Marekani, Martin Drew akiwa na wafanyakazi wa ndege wa shirika hilo. Pia Mkurugenzi wa mawasiliano wa Etihad, Deborah Flint, Ofisa Mkuu mtendaji wa kituo cha los angeles, James Hogan, Rais wa Masuala ya uhusiano na mambo ya nje wa Shirika la Makampuni ya Etihad, Hareb AL Muhairy wakifurahia baada ya uzinduzi wa Etihad Airways First & Business Class Lounge mjini Los Angeles, Marekani.

  Uzinduzi wa eneo hilo la kisasa ni kuonyesha dhamira yetu kwa Marekani na wateja wetu ukanda wa magharibi.Eneo lina huduma muhimu, likiwa na hoteli za hadhi ya juu na huduma nzuri ya hoteli.Vyakula mchanganyiko vilivyoandaliwa na wahudumu wenye uzoefu vinapatikana.

  Shirika la Ndege la ETIHAD limezindua rasmi sehemu ya kupumzika kwa daraja la kwanza na kati katika eneo la Tom Bradley katika uwanja wa kimataifa wa Los Angels. Ujenzi huo umeendana na ubora na kiwango cha huduma zinazotolewa, ikiwa ni ahadi ya huduma bora kwa wateja wa madaraja ya kwanza na kati wanaotumia ndege ya Etihad ya EY170 Boeing kutoka Marekani Magharibi na ukanda wa pwanai na kitovu cha burudani.

  Pamoja na sehemu yenye hadhi ya juu ya kupumzika ya Etihad iliyopo Washngton DC na New York, huduma hii ya kwanza Los Angles(LA) imewekwa ili kuonyesha ukarimu kwa Wamerakani, ni huduma ya kwanza katika ukanda wa Marekani Magharibi.Huduma zinazopatikana katika sehemu za mapumziko kwenye viwanja vya ndege vinavyohudumiwa na ndege za Etihad zimewekwa kuendana na utamaduni wa Kiarabu unaopatikana kwenye utamaduni wa Abu Dhabi.

  Makamu wa Rais wa Shirika la Ndege la Etihad, Martin Drew alisema” Ikiwa ndilo shirika linaloongoza kwa huduma za anga ulimwenguni, Etihad imeendelea kuboresha huduma, na kuwa kiongozi kwenye ubunifu wa huduma zake kwa wateja ndani ya ndege na wawapo sehemu ya kupandia ndege.

  “Sehemu yetu mpya ya mapumziko kwa wateja wa daraja la kwanza na la pili mjini Los Angles, imedhihirisha dhamira yetu kwa abiria wa ukanda wa marekani ya magharibi na Marekani kwa ujumla, kwa kutoa huduma bora iliyokuwa inatarajiwa na wateja wetu. Hii ni heshima kubwa kuzindua huduma hii.”

  LAWA(Los Angles World Aiprorts) na washirika wetu wa ndege wamedhamiria kuboresha huduma ndani ya ndege na kwa wageni wetu wanaosubiri kusafiri ili wapate kile kinachostahili.” Alisema Ofisa Mtendaji wa Los Angels Word Airpot.

  Sehemu hiyo ina hoteli yenye ubora pia yamewekwa mazingira ya kuwahudumia watu hata wakiwa wengi. Sehemu mpya ya mapumziko inamwezesha mteja kuwa huru, kuburudika na kufurahia huduma kutoka kwa watoa huduma wa ndege za Etihad wenye uzoefu wa kutosha.

  Kuna sehemu nzuri yenye kukufanya ujisikie vizuri ikiwa na viti vya kukaa, sehemu ya kupata mlo, bar na eneo la kutazama runinga, sehemu ya kuoga, sehemu ya matumizi ya mtandao ikiwa na soketi za kutumia USB pamoja na chumba cha magazeti na majarida ya ndani na nje ya nchi.

  Eneo maalumu limetengwa likiwa na huduma zote muhimu.

  Eneo hilo lililopo pembezoni, linaonekana kwenye eneo lenye maduka ya kisasa, hivyo sehemu hiyo ya mapumziko ya Etihad kwenye uwanja wa Los Angels imefunguliwa maalaumu kwa ajili ya wateja wa daraja la kwanza na kati wanaotumia ndege aina ya EY170.

  Huduma za Los Angels zimeongeza ubora wa huduma kwa wateja wanazozipata kwenye karibu vituo 15 ikiwamo kile cha Abu Dhabi. Miongoni mwa vituo hivyo ni kile cha Lounge and Spa kinachopatikana Terminal 3; Premium Lounges katika Terminals 1 na 3; Premium Lounge nchini Marekani), Frankfurt, London, Manchester, Dublin, Paris, Washington D.C., New York JFK, Sydney na Melbourne.

  Huduma za ndege za Etihad limekuwa likitoa huduma zake kati ya Los Angeles Na Uwanja wa Kimataifa wa Abu Dhabi tangu Julai Mosi 2014. Vilevile huduma za usafiri wa anga zinatolewa kati ya Abu Dhabi na maeneo ya Chicago, San Francisco na Washington, D.C pamoja na safari mbili kwa siku New York na mara tatu kwa wiki Dallas/Fort Worth.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAZINDUA VYUMBA VYA MAPUMZIKO VYA KISASA UWANJA WA KIMATAIFA WA LOS ANGELES Rating: 5 Reviewed By: MICHUZI BLOG
  Scroll to Top