JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAANZISHA HUDUMA YA NDEGE YA KISASA SHANGHAI.

Share This
§  Wateja watashuhudua huduma za ubora wa hali ya juu kutoka kwa watoa huduma.
§  Itaongeza asilimia 27 ya ongezeko la ukuaji kibiashara kati ya Shanghai-Abu Dhabi.
§  Abu Dhabi inaunganisha zaidi ya mataifa 40 eneo la Ghuba, Ulaya, Afrika na Amerika Kusini.

Shirika la Ndege la Etihad limeanzisha safari mpya ya ndege yake ya kisasa ya Boeing 787 Dreamliner kwenda Shanghai kutoka Abu Dhabi. Ndege hiyo yenye ubora wa kiwango cha juu kwa daraja la kati na kwanza pamoja na wahudumu waliobobea, ina jumla ya viti 299 ambapo daraja la kwanza ina viti 28 na daraja la kati kuna viti 271 ikiwa na uwezo wa kufanya safari nane ikiwakilisha ongezeko la asilimia 14 katika safari zake

Ndege ya Etihad EY862 kutoka Abu Dhabi iliondoka saa nne na dakika 25 Agosti 02 ikitokea Mashariki ya kati na kuwasili Shanghai saa tano na dakika kumi asubuhi ya tarehe 03 Agosti. Ndege hiyo iliyozindua safari zake iliondoka tena Agosti 03 saa sita kamili mchana siku hiyo hiyo. Sherehe hiyo ya uzinduzi ilihudhuriwa na wadau wa usafiri wa anga waliopo nchini China.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Etihad, Peter Baumgartner alisema,”Tangu kuzinduliwa usafiri wa anga kati ya Shanghai na Abu Dhabi katika kipindi cha miaka minne iliyopita, tumeshuhudia ukuaji mkubwa katika sekta ya utalii nchini China na kuongezeka kwa wateja.”

Uamuzi wa kuongeza ndege ya kisasa ya Boeing 787 inatokana na umuhimu wa sekta ya anga kati ya Shanghai na Abudhabi. Shanghai ni mji wa kisasa unaokua kwa kasi kiuchumi, kibiashara, usafirishaji kwa bandari jambo ambalo limeisukuma Shirika la Etihad kuwa kiungo muhimu kwa kuanzisha ndege mpya ya kisasa katika eneo hili.

Bwana Baumgartner aliongeza, “Huduma za Ndege mpya ya Boeing 787 itasaidia kuvutia na kukuza utalii ndani na nje ya Shanghai na miji inayoizunguka mashariki mwa China. Kwa kuongeza hii itawezesha ukuaji wa biashara China na wateja kufurahia huduma bora ya usafiri wa ndege ya kisasa kwa kuwaunganisha na Abu Dhabi na mataifa zaidi ya 40 Ukanda wa Ghuba, Ulaya, Afrika na Amerika Kusini.

Kwa mujibu wa Global Business Travel Association, China ndiyo taifa linaloongoza katika soko la kibiashara ukiacha Marekani ambapo iliwekeza zaidi ya Dola za kimarekani milioni 291.2 katika mwaka 2015. Ndege hiyo ya kisasa itawezesha Shirika la Ndege la Etihad kuimarika kibiashara katika jamii ya China kwa kuanzisha ndege ambayo itawavutia wateja wa aina mbalimbali kwenye soko la usafiri wa anga.

Wateja watajipatia huduma zote muhimu wanapokuwa kwenye sehemu za mapumziko na baada ya ndege kutua. Kuna huduma ya mapumziko inayopatika kwenye miji zaidi ya 30 ikiwamo Beijing na Shanghai. Wawapo katika Uwanja wa Kimataifa wa Abu Dhabi, wageni hupatiwa huduma bora zenye ubora wa hali ya juu kupitia sehemu maalumu walizotengewa kupumzika huku wakifurahia huduma inayotolewa kupitia eneo maalumu kwa wateja wa daraja la kwanza na  kutoka kwa wakala wa huduma wa Shirika wa Etihad (EAP).

Katika ndege hiyo mpya, kwenye daraja la kati kuna eneo ambalo litamwezesha mteja kupata huduma mbaliambali ikiwamo runinga yenye ukubwa unaomwezesha kuona vyema, pia kuna nafasi ya kutosha kumwezesha mteja kuwa huru.

Pia, kuna viti ambavyo vinampa uhuru wa kukaa na kuna mifumo ambayo inamwezesha mteja kusogeza kiti kwa kadiri anavyohitaji. Na kila chumba maalumu kwenye ndege hiyo kuna runinga ya kisasa ikiwa na vidhibiti sauti.

Wageni wanaotumia usafiri wa daraja la kati, wanayo fursa ya kuchagua chakula wanachotaka jambo linalowapa nafasi kuchagua wanachotaka wawapo safarini. Kila daraja lina huduma maalaum ya kutoka kwa watoa huduma wa Etihad. Aidha wateja wanakuwa na wigo wa kuchagua chakula wakipendacho kutoka wa wasimamizi wa vyakula na watoa huduma hao hutoa msaada wa karibu kwa  wazazi ambao huwa wanasafiri na watoto.

Mathalan kwenye ndege hiyo, burudani inapatikana. Kuna mfumo wa muziki wa kisasa wa Panasonic eX3 IFE ambao unapatikana kwenye ndege ya Boeing 787s na Airbus A380s.

Mteja ataweza kufurahia mfumo wa bure wa intanteti kwa ajili ya simu na kumwezesha pia kutazama chaneli mbalimbali za runinga kipitia satellite ikiwa ni matangazo ya moja kwa moja.

Kwa wateja wa daraja la kati, ndege hiyo ina viti vyenye ubora ambavyo kuna vifaa maalumu vya kusikilizia muziki, pia viti vyake vikiwa na nafasi ya kutosha kwa kila mtu kukaa kwa uhuru huku akiburudika na televisheni inayopatikana kwa kila kiti.

Ndege imetengenezwa ikiwa na vifaa vya kudhibiti unyevunyevu pamoja na mgandamizo wa hewa ili kumfanya mteja ajisikie vyema awapo safarini.

Shanghai ni sehemu ya saba kufikiwa na huduma ya ndege hiyo ya kisasa ya B787-9 Dreamliner. Maeneo mengine ambako ndege ya aina hiyo inafanya safari zake ni Perth, Brisbane, Singapore, Washington DC, Zurich na Düsseldorf.
Shirika la Ndege la Etihad kwa mara ya kwanza lilizindua safari zake mara tano kwa wiki  kwa kutumia ndege ya A330-220 kwenda Shanghai tangu Machi 2012.

Ratiba kwa ndege za Abu Dhabi-Shanghai:

NAMBA YA NDEGE.
MAHALI INAPOTOKA
KUONDOKA
INAPOKWENDA
KUWASILI
KIPINDI
AINA YA NGEGE
EY862
Abu Dhabi
(AUH)
22:25
Shanghai
(PVG)
11:10 next day
Daily
B787-9
EY867
Shanghai
(PVG)
00:30
Abu Dhabi (AUH)
06:15
Daily
B787-9


Zingatia: Safari zote za kuondoka na kuwasili zimewekwa kulingana na muda wa eneo husika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad