728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, August 4, 2016

  Serikali yaombwa Kuubariki Mradi wa ECO ENERGY Wilayani BAGAMOYO


  Na Saleh Masoud, BAGAMOYO

  Kikundi cha wakulima wa zao la miwa kilichopo Kiwangwa Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wameiomba Serikali ya awamu ya tano kuruhus Mradi wa ECO ENERGY utakaowezesha kujengwa kwa kiwanda cha sukari maeneo hayo.

  Katika Kikao cha Wadau wa Zao hilo Wakulima hao, wametilia Shaka kusuasua kwa Ujenzi wa Kiwanda hicho cha kuzalisha sukari, ambapo wamesema kukawia kwa Mradi wa ECO ENERGY kutazidi kuwadidimiza Kimaisha na kurudisha nyuma maendeleo yao Kiuchumi.

  Wamesema Tumaini walilonalo kwa sasa kuona mradi wa ECO ENERGY ukianza kufanya Kazi mara moja, ambapo watakuwa na fursa pana ya kuuza zao la Miwa kwa mwekezaji atakayejenga kiwanda cha zao hilo katika Wilaya ya BAGAMOYO.
  Mwenyekiti wa Kikundi cha CHUHA Bi PILI ALLY akielezea Changamoto zinazowapata wakulima Wadogo wa zao la Miwa Wilayani Bagamoyo, baada ya Kuchelewa kuanza kwa Mradi wa ECO ENERGY utaowezesha Kujengwa kwa Kiwanda cha Sukari Katika Wilaya Hiyo.

  Kuhusu tuhuma zinazotolewa na Wadau wa masuala ya Mazingira kuhusu Kilimo cha Miwa kwenye Ukanda huo, wameiomba Serikali iliyo chini ya Rais Dkt JOHN MAGUFULI kutuma wachunguzi ambao wamebobea kwenye suala la Mazingira ili kujiridhisha na kutoa Baraka za kuanza kwa Mradi wa ECO ENERGY.

  Kwa Upande wake mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Kiwangwa akizungumzia juu ya tatizo hilo amesema vilio vya wakulima katika eneo lake ni vyema vikatafutuwa ufumbuzi wa haraka.

  Amesema kushughulikia mapema mgogoro huo kutawasaidia Wakulima hao wadogo waliokopa fedha kwenye taasisi za Kibenki kurejesha mikopo hiyo baada ya kuuza zao Miwa kwa mwekezaji wa Kiwanda kitakachojengwa baada ya Kuanza kwa Mradi wa ECO ENERGY.

  Wakati malalamiko hayo ya wakulima yakitolewa uongozi wa mradi wa ECO ENERGY unaosimamia mradi huo, Umesema tayari wameanza kupata hasara ya Kutupa Miwa ambayo imevunwa lakini hakuna sehem ya kuipeleka kwa sababu ya kukosekana kwa Kiwanda kutokana na kusuasua kwa mradi huo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Serikali yaombwa Kuubariki Mradi wa ECO ENERGY Wilayani BAGAMOYO Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top