728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, August 19, 2016

  SERIKALI YAAINISHA MKAKATI WA KUWAELEZA WANANCHI UTEKELEZAJI WA AHADI ZAKE


  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Hassan Abbasi akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo kueleza mikakati ya kuimarisha mawasiliano kati ya Serikali na wananchi kupitia utoaji wa taarifa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuhusu utekelezaji wa ahadi za Serikali ya Awamu ya Tano. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo upande wa Habari Bw. Vincent Artemony Tiganya.

  Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa ukitolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Hassan Abbasi, juu ya mikakati ya Serikali katika kuimarisha mawasiliano kati ya Serikali na wananchi kupitia utoaji wa taarifa mbalimbali za utekelezaji wa ahadi za Serikali ya Awamu ya Tano

  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Hassan Abbasi akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo kueleza mikakati ya kuimarisha mawasiliano kati ya Serikali na wananchi kupitia utoaji wa taarifa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuhusu utekelezaji wa ahadi za Serikali ya Awamu ya Tano.Picha/ Aron Msigwa


  Na. Immaculate Makilika - Dar es salaam.

  Serikali imesema kuwa itaanza kutekeleza mikakati mbalimbali inayoloenga kuwapatia wananchi taarifa za kila mara kuhusu utekelezaji wa ahadi zake

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO Bw. Hassan Abbasi alisema kuwa Serikali imeandaa mikakati ambayo itasaidia kuongeza uwazi na ushirikishaji ili kuwawezesha wananchi kupata mbalimbali taarifa kwa wakati.

  “ Mawaziri wote wataanza kuonekana kwenye vyombo vya habari kuanzia wiki ijayo wakielezea vipaumbele na kuainisha mafanikio na changamoto za utekelezaji wa mipamgo na sera mbalimbali na hili ni zoezi endelevu” alisema Bw. Abbasi. Aliongeza kuwa, lengo ni kutoa taarifa ya utekelezaji kwa wananchi kuhusu mipango mbalimbali ya Serikali kupitia wizara ambapo wataelezwa kuhusu vipaumbele vya wizara na nini kinafanyika.

  Bw. Abbasi, ametaja mikakati hiyo kuwa ni kuboresha mfumo wa Mawaziri na Watendaji waandamizi wa serikali kuzungumza na wananchi ili kuanisha utekelezaji wa vipaumbele vya bajeti, sera na mipango ya Taifa inayosimamiwa na Wizara husika.

  Aidha, mkakati mwingine ni kuanzisha utaratibu wa Idara ya Habari- MAELEZO kueleza kwa umma kila mara kuhusu utekelezaji wa sekta zote katika ngazi ya kitaifa ambapo hivi karibuni Msemaji wa serikali atakuwa akitoa taarifa hizo.

  Akizungumzia kuhusu mpango wa kuimarisha mahusiano na wadau mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari Bw. Abbasi alisema kuwa Idara ya Habari -MAELEZO imejipanga kufanya kazi kwa karibu ili kuhakikisha kwa pamoja wanaleta mapinduzi katika sekta ya Mawasiliano nchini.

  Mawaziri wanatarajiwa kutoa taarifa kwa umma kupitia vyombo mbalimbali vya habari kuanzia Agosti 25 mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: SERIKALI YAAINISHA MKAKATI WA KUWAELEZA WANANCHI UTEKELEZAJI WA AHADI ZAKE Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top