728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, August 31, 2016

  SEKTA YA UJENZI,VIWANDA USAFIRISHAJI NA MIGODI ZINAONGOZA KWA AJALI -OSHA

  AKALA wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA) imesema sekta zinazongoza kuwa na ajali kazini ni sekta ya Ujenzi, viwanda usafirishaji na migodi.

  Hayo ameyabainisha leo jijini Dar es Salaam Mtendaji Mkuu wa OSHA Dk. Akwilina Kayumba wakati waakiadhimisha miaka 15 ya kuanzishwa kwa Wakala huo kwa kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Rufaa ya Mwanamyamala.

  Alisema wamekuwa wakipokea taarifa kutoka kwa wadau mbalimbali wa sekta hizo hivyo kwa sasa hali bado sii nzuri.

  “Tunakabiliwa na changamoto nyingi kwa sasa ikiwepo iadadi isiyotosha ya watumishi ukilinganisha na mahitaji ya nchi na uhaba wa majengo ya ofisi kwa nchi nzima tuna ofisi kumi tu ambapo tunatakiwa kutoa huduma kila mahali na wadau wetu wote wanahaki ya kupata huduma mahali popote alipo,”alisema Dk. Kayumba.

  Alitaja changamoto nyingi uelewa wa masuala ya afya na usalama baina ya wadau haujaridhisha, kwa kuwa wafamyakazi wengi hawana uelewa wa hali ya juu kuhusu usalama na afya wawapo kazini.

  Dk.Kayumba alisema katika kuelekea Tanznia ya viwanda lazima wadau wanunue vifaa kwa ajili ya kujilinda mahali pa kazi ili kupunguza ajali hizo. Alisema baadhi ya mafaniko waliyopata pamoja na kuanzishwa kwa kozi ya Taifa ya Afya na Usalama mahali pa kazi kwa maafisa ambapo hadi sasa idadi ya wahitimu imifika 1,800.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: SEKTA YA UJENZI,VIWANDA USAFIRISHAJI NA MIGODI ZINAONGOZA KWA AJALI -OSHA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top