728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, August 22, 2016

  Rais wa zamani Kenya Mwai Kibaki alazwa Afrika Kusini

   
  Aliyekuwa Rais wa Kenya Mwai Kibaki, 84, amelazwa hospitalini nchini Afrika Kusini akipokea matibabu maalum baada ya kuugua mwishoni mwa wiki.

  Kiongozi huyo wa zamani aliugua akiwa nyumbani kwake na akapelekwa hospitalini Karen, Nairobi Jumamosi jioni kabla ya kusafirishwa Afrika Kusini Jumapili.

  "Aliandamana na daktari wake. Tunamtarajia arejee nyumbani hivi karibuni, na Wakenya watafahamishwa kuhusu hali yake wakati mwafaka," taarifa iliyotolewa na familia yake ilisema.

  Desemba mwaka 2002, Bw Kibaki aliumia baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani wakati wa kampeni na akapelekwa Uingereza kwa matibabu.
  Aliapishwa kuwa rais muhula wake wa kwanza akiwa kwenye kiti cha magurudumu.

  chanzo BBC
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Rais wa zamani Kenya Mwai Kibaki alazwa Afrika Kusini Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top