728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, August 31, 2016

  Rais Magufuli mgeni rasmi Kongamano la Afya

  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
  Dar es Salaam.
  31/08/2016.

  RAIS Dkt. John Magufuli anatarajia kuwa mgeni rasmi katika  kongamano la tatu la kitaifa la afya  litakalofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 14-15 Novemba, mwaka huu.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Rais wa Taaasisi ya Tanzania Health Summit (THS) Dkt. Omary Chillo alisema kuwa kongamano hilo litahudhuriwa na  wadau 500 wa afya kutoka ndani na nje ya Tanzania wakiwemo watoa huduma za afya, watunga sera, watafiti wa magonjwa ya afya, wachumi, na wadau wa maendeleo.

  Alisema kongamano hilo litalenga kuongeza nguvu za Serikali za kuboresha afya za Watanzania kupitia kupashana habari na ujuzi, majadiliano ya changamoto na kufikia muafaka wa njia bora za utatuzi wake ili kuimarisha huduma za afya nchini.

  Aidha, alisema kuwa mkutano huo utahusisha vipengele mbalimbali ikiwemo vikao vya mashauriano yatakayogusa mada mbalimbali za maendeleo ya afya, taarifa kutoka kwa wataalamu wabobezi wa afya, pamoja na kuwasilisha matokeo ya uchunguzi.

  Pia aliongeza kuwa katika kongamano hilo pia kutakuwa na maonyesho ya huduma na bidhaa kutoka kwa wasambazaji wa huduma za afya ya mashirika ya umma na binafsi.

  Dkt. Chilo alitoa wito kwa wadau wa afya nchini kutoka Serikalini, mashirika binafsi, mahospital, asasi zisizo za kiserikali, taasisi za kitaaluma, wasambazaji, na washirika wa maendeleo kushiriki kikamilifu katika kongamano hilo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Rais Magufuli mgeni rasmi Kongamano la Afya Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top