728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, August 25, 2016

  Rais Magufuli amteua Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Agosti, 2016 amemteua Bw. Andrew Wilson Massawe kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

  Kabla ya uteuzi huo Bw. Andrew Wilson Massawe alikuwa Mkurugenzi wa Mifumo ya Kompyuta katika Benki Kuu Tanzania (BOT).

  Bw. Andrew Wilson Massawe anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Modestus Francis Kipilimba ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

  Uteuzi wa Bw. Andrew Wilson Massawe unaanza mara moja.


  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es Salaam
  25 Agosti, 2016
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Rais Magufuli amteua Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top