728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, August 31, 2016

  BW.GERSON MSIGWA ATHIBITISHWA KUWA MKURUGENZI WA MAWASILIANO IKULU

  Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, (Director of Presidential Communication - DPC). Bw. Gerson Partinus Msigwa,aliyethibitishwa leo na Rais Dkt John Pombe Magufuli


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemthibitisha Bw. Gerson Partinus Msigwa kuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, (Director of Presidential Communication - DPC).

  Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Agosti 31,2016 na Katibu Mkuu Ikulu Bw. Peter Ilomo imeeleza kuwa Bw. Gerson Partinus Msigwa amethibitishwa kuanzia leo tarehe 31 Agosti, 2016 kushika wadhifa huo.

  Kabla ya uthibitisho huo, Bw. Gerson Partinus Msigwa alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, katika Ofisi ya Rais Ikulu kuanzia tarehe 17 Novemba, 2015.

  Jaffar Haniu
  Kaimu Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi.
  Dar es Salaam
  31 Agosti, 2016
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: BW.GERSON MSIGWA ATHIBITISHWA KUWA MKURUGENZI WA MAWASILIANO IKULU Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top