728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, August 29, 2016

  PROF WANGWE ATAKA WATANZANIA KUENDELEA KUMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI

  PROF WANGWE

  Na Daudi Manongi,MAELEZO

  Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii Prof Samwel Mwita Wangwe amesema kuwa uongozi wa Awamu ya Tano umefanya kazi kubwa katika kuweka maslahi ya Taifa mbele ikiwamo kuongezeka kwa bajeti ya maendeleo na kupunguza matumizi ya serikali.

  Hatua hii imesaidia nchi kusonga mbele kupitia uboreshaji wa utendaji kwa watumishi wa umma na hivyo kujenga imani kubwa kwa wananchi juu ya Serikali yao.Profesa Wangwe ametoa kauli hiyo leo mjini Dar es salaam wakati akitoa tathmini ya uongozi wa Awamu ya Tano.

  Amesema kuwa Rais Magufuli katika uongozi wake umesaidia kuokoa fedha nyingi za walipa kodi ambazo zilikuwa zikiishia mikononi mwa watu wachache na kuzielekeza katika shughuli nyingine za maendeleo.

  Profesa Wangwe amewataka wananachi kumuunga mkono Rais Magufuli kwenye harakati zake za kupambana na matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kuwa matokeo yake yatasaidia kuijenga Tanzania mpya ambayo kila mwananchi atapata fursa kunufaika na rasilimali za nchi.

  “Kwa kweli Rais huyu amefanya mabadiliko makubwa sana na kwa sasa nchi imerudi katika hali nzuri, kwani nchi ilikuwa imefika mahali pabaya na kwa hiyo aliona ni budi kuhakikisha Rushwa na Ufisadi vinakomeshwa na kwa hili ameanza vizuri na nchi inakwenda katika mwongozo mzuri kwani ameboresha utendaji kazini serikalini na kubana matumizi ambayo yamesaidia kuokoa pesa nyingi ambayo inatumika katika maendeleo ya nchi hii”aliongeza Profesa Wangwe.

  Mbali na hayo Profesa Wangwe ameshauri Serikali kuweka mfumo mzuri katika ukusanyaji kodi kwa kurasimisha biashara ili mfumo huu wa EFD utumike kirahisi na pia kutengenezwe mazingira mazuri ya biashara kwa kuweka mazingira rahisi ya kuandikisha biashara kwani huchukua muda mrefu kwani kwa kufanya hivyo kasi ya kurahisisha utendaji na wafanyabiashara watalipa kodi kwa wingi na uchumi utakua.

  Pia Profesa Wangwe ametoa ushauri kwa vyama vya upinzani kuacha na na maandamano yasiyo na tija na badala yake wakae chini na kuzungumza na serikali ilikupata mwafaka na hivyo amani iendelee kuchanua katika nchi hii.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: PROF WANGWE ATAKA WATANZANIA KUENDELEA KUMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top