728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Sunday, August 28, 2016

  PEACOCK HOTEL YAZINDUA RASMI MTANDAO WAKE WA KIJAMII UNAOLENGA KUTANGAZA CHAKULA CHA ASILI CHA MTANZANIA.


  Mmoja kati ya Wakurugenzi wa Peacock Hotel,Daniel Mfugale akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uzinduazi wa mtanao wa kijaamii unaolenga kutangaza chakula cha asili cha Mtanzania leo jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya wafanyakazi wa hotel hiyo waliofika kwenye uzinduzi huo leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii).

  Uongozi wa Peacock Hotel umezindua rasmi mtandao wake wa kijaamii unaolenga kutangaza chakula cha asili cha Mtanzania.

  Mmoja kati ya Wakurugenzi wa Hotel hiyo Daniel Mfugale alisema kuwa uamuzi huo umefanyika baada ya kuona mitandao ya kijamii sasa inasambaza taarifa haraka na kuwafikia watu wengi nje na nchi hivyo itasaidia kuongeza utalii Nchini.

  “Kwa sasa mitandao ya kijamii ndiyo imeshika hatamu kwa usambazaji wa taarifa hivyo huduma yetu iitwayo Usiku wa Mtanzania ambayo ni maalumu kwa chakula cha asili cha makabila yote nchini itakua inatangazwa katika kurasa zetu za facebook na Instagram tulizozifungua leo”, alisema Mfugale.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: PEACOCK HOTEL YAZINDUA RASMI MTANDAO WAKE WA KIJAMII UNAOLENGA KUTANGAZA CHAKULA CHA ASILI CHA MTANZANIA. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top