728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, August 5, 2016

  NYOSHI EL SADAT AHIDI KUWAPAGAWISHA WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA ONESHO LA KUMSAKA MISS KANDA YA KASKAZINI KESHO

  Na Woinde Shizza ,Arusha.
   
    Rais Wa bendi ya FM Academia Nyoshi El Sadat amewahidi wakazi Wa jiji la Arusha kuwapa burudani ya nguvu katika onyesho la kumsaka Miss Kanda ya kaskazini.

  Akiongea na waandishi Wa habari jijini hapa, Mwanamuziki huyo alisema kuwa bendi hiyo imejipanga vya kutosha kuwapa burudana wapenzi na mashabiki wake.Alisema kuwa katika shoo hiyo ya Usiku Wa kumpata mrembo Wa kanda ya kaskazini amekuja na wanamuziki wote pamoja na wacheza show wa bendi ya Fm Academia .

  "Tunawapa burudani ya kufa mtu tunamastaili mapya ,pia yule mnenguaji ambae walimmiss kwa muda mrefu Qeen Suzy atakuwepo katika onyesho hilo"alisema Nyoshi .

  Naye mwandaaji wa onyesho hilo Faustine Mwandago alisema kuwa katika show hii atahakikisha washabiki wote wanaifurahia show hiyo . Alisema show hiyo itafanyika kesho jumamosi July sita itaanza kuanzia tatu kamili Usiku na kiingilio kawaida itakuwa kawaida 10000 huku V.I.P 30000.

  Picha ikionyesha warembo wanaoshiriki shindano la miss kanda ya kaskazini wakiwa wanafanya mazoezi kwa ajili ya shindano linalofanyika jumamosi hii July 6 katika viwanja vya ukumbi Wa triple A .
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: NYOSHI EL SADAT AHIDI KUWAPAGAWISHA WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA ONESHO LA KUMSAKA MISS KANDA YA KASKAZINI KESHO Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top