Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii (NSSF)Prof Godius Kahyarara (kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya pesa yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 2 na laki 1 (zaidi ya Tsh bilioni nne) kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) Dkt Samuel Nyantahe (wa tatu kushoto) ikiwa ni mkopo kwa ajili ya kuongeza uzalishaji kwenye kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu cha Tanzania Biotech Product Ltd kilichopo wilayani Kibaha, mkoani Pwani wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (katikati), Mkuu wa wilaya ya Kibaha, Bi Assumpta Mshana, (wa pili kulia) Mkurugenzi wa huduma za sheria wa Benki ya Azania, Bw Geofrey Dimoso (wa pili kushoto) na Kaimu Meneja Mkuu wa kiwanda hicho Bw Samwel Mziray.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama Mkuu wa wilaya ya Kibaha, Bi Assumpta Mshana pamoja na jopo la maofisa kutoka NSSF, NDC, benki ya Azania na uongozi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu cha Tanzania Biotech Product kwa pamoja wakimsiliza mmoja wa wataalam kutoka kiwanda hicho aliekuwa akifafanua moja ya shughuli za kiwanda hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii (NSSF)Prof Godius Kahyarara (kushoto) pamoja na viongozi wa NSSF kwenye ziara hiyo.
Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii.
SHIRIKA
la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limetoa mkopo wa dola za Kimarekani
mil. 2.1 (zaidi ya sh bilioni nne) kwa kiwanda cha kuzalisha
viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu cha Tanzania Biotech Product Ltd
kilichopo wilayani Kibaha, mkoani Pwani ili kukiongezea uzalishaji wake,
hatua inayotajwa kuwa ni kuitikia wito wa Rais Dr John Magufuli wa
kuifanyaTanzania kuwa nchi ya viwanda.
Mbali
na mkopo huo unaotolewa kupitia benki ya Azania itayayosimamia
urejeshwaji wake, pia shirika hilo lipo kwenye mchakato wa kuwekeza
kwenye ujenzi wa viwanda vipya na vikubwa zaidi vya kutengezeza nguo,
matairi pamoja na sukari hapa nchini.
Akizungumza
kwenye hafla hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,
Ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama mbali na kulipongeza
shirika hilo kwa kuunga mkono nia ya Rais na serikali kwa ujumla katika
kuelekea uchumi wa viwanda, alisema uwezeshaji wa kiwanda hicho
umeongeza kasi ya vita dhidi ya ugonjwa wa Malaria kwa asilimia tisini
(90).
“Kiwanda
kipekee barani Afrika na ufanisi wake utawanufaisha si tu watanzania
bali Waafrika kwa ujumla na kutuletea fedha za kigeni, na kuweza
kufikia uchumi wa kati katika sekta ya viwanda’’ alisema.
Amesema
uamuzi wa shirika hilo kutoa mkopo huo kupitia benki ya Azania
utaliwezesha shirika hilo kuwa na msimamizi thabiti wa marejesho ya pesa
za wanachama wa mfuko huo.
“Mwanzo
kabisa kwenye uamuzi huu niliomba kupata uhakika fedha za wanachama na
nilipohakikishiwa kuwa kuna benki itasimamia mkopo huu basi nikajua
pesa za wanachama zipo salama. Niendelee tena kuwaomba wahusika wote
wawe makini kwenye pesa hizi,’’ alisisitiza.
Alitoa
wito kwa mifuko ya hifadhi hapa nchini kuhakikisha inawekeza zaidi
kwenye viwanda huku akiwataka viongozi wa mashirika mbalimbali
kuhakikisha wanalinda haki na maslahi ya wafanyakazi wao likiwemo suala
la kuwaunganisha wafanyakazi wao na mifuko ya hifadhi ya jamii.
Akizungumza
wilayani Kibaha wakati wa hafla fupi ya kukabidhi mkopo huo kwa
Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) linalomiliki kiwanda hicho,
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara alisema shirika lake lina
dhamira ya dhati katika kuwekeza kwenye viwanda nchini ili kuongeza
fursa za kiuchumi kwa wananchi wa Tanzania.
“Pamoja
na kuitikia wito wa Rais Dk.John Magufuli katika kuibadilisha Tanzania
kuwa nchi ya viwanda ili kuiongeza ajira hapa nchini lakini pia
tunatarajia kupata faida kupitia marejesho ya pesa hizi,’’ Alibainisha.
Akiwatoa
hofu wanachama wa mfuko huo na watanzania kwa ujumla kuhusu usalama wa
pesa zao, Prof Kahyarara alisema uamuzi wa shirika kuwekeza kwenye
viwanda sio mgeni kwa kuwa ulianza miaka ya nyuma ambapo shirika hilo
liliwezesha viwanda vya saruji Mbeya, Mkonge Tanga, Sukari Kagera na
kiwanda cha nguo 21st Century cha Morogoro.
“Uwekezaji
huo ulionyesha mafanikio makubwa kwa wananchi wengi walipata ajira na
shirika lilipata faida iliyokusudiwa na kuboresha mafao ya wananchama.
Tupo makini na aina za uwekezaji na miongoni mwa kanuni tunazotumia
katika uwezaji ni suala la tija, faida, usalama na malengo ya mradi
husika hususani katika kuinua uchumi wa nchi kwa ujumla,’’ alisema.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya NDC Dkt Samuel Nyantahe alisema mkopo
huo utakiwezesha kiwanda hicho ambacho kimejengwa kwa kushirikiana na
kampuni ya LABIOFAM SA ya nchini Cuba kupanua uzalishaji wake na kuwa
katika nafasi ya kutafuta soko hadi nje ya nchi.
Naye
Mkurugenzi wa huduma za sheria wa Benki ya Azania, Bw Geofrey Dimoso
alisema benki yake imejipanga kuhakikisha inasimamia urejeshwaji wa pesa
hizo kwa mfuko wa NSSF huku akiwatoa hofu wanachama wa mfuko huo kuwa
pesa zao zipo salama.
No comments:
Post a Comment