728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, August 5, 2016

  NHIF HAKIKISHENI WANANCHI WANAHAMASISHWA NA KUELEWA FAIDA ZA KUJIUNGA NA CHF- SIMBACHAWENE

   Waziri ofisi ya Raisi (TAMISEMI), George Simbachawene (MB) akisisitiza mfuko kuendelea kupanua wigo wa elimu kwa wananchi waelewe faidia za kujiunga na CHF ili  kuongeza kasi ya uboreshaji wa huduma kama ilivyokusudiwa na serikali ya awamu ya tano(5) kuwa  ifikapo Juni, 2020 asilimia 30% ya watanzania wawe wamejiunga na bima ya afya,mbele ya waandishi wa habari wakati alipotembelea banda la NHIF katika maonesho ya nane nane yanayofanyika kitaifa kwenye viwanja vya  Ngongo mjini Lindi.anayemsikiliza mbele ni Meneja wa mfuko huo mkoa wa Lindi Fortunata Raymond.
  Meneja wa mfuko wa taifa wa bima ya afya, Fortunata Raymond akitoa taarifa ya huduma mbalimbali  zinazotolewa kwenye banda la mfuko kwa Waziri ofisi ya raisi (Tamisemi) Mhe.George Simbachawene MB.ambapo hadi sasa wanachi na wananchama wa mfuko takribani 600 waliweza kupatiwa huduma za upimaji.
   Mtaalamu wa upimaji wa saratani ya matiti kwenye banda la NHIF Dkt. F.Malibiche akitoa ufafanuzi kwa mgeni rasmi waziri ofisi ya raisi (TAMISEMI), George Simbachawene (MB),takribani akina mama 113 na wanaume 5 waliweza kupimwa na kutogundulika na viashiria vya saratani
  Waziri ofisi ya Rais (TAMISEMI), George Simbachawene akipima BMI wakati alipotembelea banda la bima ya afya,wanaoshuhudia kulia mwenye kofia ya kijani Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: NHIF HAKIKISHENI WANANCHI WANAHAMASISHWA NA KUELEWA FAIDA ZA KUJIUNGA NA CHF- SIMBACHAWENE Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top