728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, August 4, 2016

  NEWZ ALERT:RAISI WA SIMBA EVANCE AVEVA ASHIKILIWA NA POLISI, TAKUKURU WAENDELEA NA UCHUNGUZI

  Na Zainab Nyamka.

  KAMANDA  wa polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni, ACP Christopher Fuime amethibitisha kumshikilia rais wa klabu ya Simba na alipoulizwa ni tuhuma gani zinazomkabili kiongozi huyo wa juu kabisa wa wekundu wa Msimbazi alisema ni vizuri swali hilo wakiulizwa TAKUKURU. Tumemshikilia toka juzi jioni na juhudi za kupatiwa dhamana zimeshindikana mpaka dakika hii kwani sisi kazi yetu ni kumshikilia tu ila mamlaka zaidi yapo TAKUKURU.

  Aveva anashikiliwa na polisi kwa kibali cha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU lakini bado haijafahamika moja kwa moja anakabiliwa na tuhuma gani huku baadhi ya watu wakidai ni matumizi mabaya ya fedha walizolipwa kutoka Etoile Du Sahel juu ya malipo ya Emanul Okwi pamoja na za Mbwana Samatta ambazo anadaiwa kuzihamisha kutoka kwenye akaunti ya klabu ya Simba.

  “Kwa upande wangu siwezi kujua ila kwa maelezo zaidi  TAKUKURU wanaweza wakajua na ni lini huo uchunguzi  utakamilika na kumpeleka mahakamani. Sisi tunamshikilia kwasababu TAKUKURU hawana mahabusu binafsi,  na maswali yote  wangejibu sababu hasa ya kushikiliwa kwa Evance Aveva,” amesema Fuime

  Kwa upande wa TAKUKURU kupitia afisa habari Musa Misalaba amesema kuwa Aveva yupo kwenye mikono salama na wanamshikilia kwa uchunguzi, kwa sasa wanaendelea na uchunguzi kwani sheria inaturuhusu kufanya uchunguzi  na pia tunaruhusiwa kukamata, kupekuwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: NEWZ ALERT:RAISI WA SIMBA EVANCE AVEVA ASHIKILIWA NA POLISI, TAKUKURU WAENDELEA NA UCHUNGUZI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top