728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, August 5, 2016

  NAIBU WAZIRI WA ELIMU MH. MHANDISI STELLA MANYANYA AWA MGENI RASMI MAHAFALI YA BROOKHOUSE INTERNATIONAL SCHOOL JIJINI DAR


  Mgeni Rasmi katika mahafali ya Shule ya awali ya Brookhouse International School Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mh. Mhandisi Stella Manyanya akimpa mmoja wa watoto cheti cha kuhitimu Elimu ya awali
  Watoto wahitimu wa Shule ya awali wakiendelea kupokea Vyeti vyao
  Baadhi ya watoto wahitimu wa shule ya awali wakipata picha ya pamoja na mgeni rasmi .
   
  Mh. Mbunge wa Jimbo la Kawe Halima Mdee akiwa katika mahafali hayo
  Mgeni Rasmi katika mahafali ya Shule ya awali ya Brookhouse International School Naibu Waziri wa Elimu Mh. Mhandisi Stella Manyanya akiadhimisha siku yake ya Kuzaliwa hapa akimlisha keki Mkurugenzi mkuu wa Shule hiyo Mary Shirima


  Mgeni Rasmi katika mahafali ya Shule ya awali ya Brookhouse International Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mh. Mhandisi Stella Manyanya akitoa Hotuba kwa wanafunzi pamoja na wageni waalikwa
  Mwalimu wa Taaluma wa Brookhouse International School Omega Kessy akitoa neno la utangulizi wakati wa mahafali hayo.

  Mwalimu Mkuu wa Sunrise Nursery and Primary School Bw. Onesphor Vitalis akitoa utambulisho kwa wageni waalikwa waliofika katika Mahafali hayo ya shule ya awali.
  Mkurugenzi Mkuu wa Sunrise Nursery and Primary School Bi. Marry Shirima akitoa maelezo ya kina juu ya shule hiyo, kumshukuru mgeni rasmi kufika katika mahafali hayo ya watoto wa shule ya awali pamoja kuwapongeza kwa kuhitimu
  Wahitimu wa Shule ya awali wakionesha uwezo wao wa kusoma kwa makini

  Wahitimu wa Shule ya awali wakionesha uwezo wao wakitoa Burudani kwa kucheza moja ya ngoma za asili za hapa Tanzania


  Mshehereshaji katika mahafali hayo Mwalimu Isaria akiendelea kutoa utaratibu wakati wa Sherehe hizo


  Watoto wa Shule ya awali ya Brookhouse International School ambao wanandoto ya kuja kuwa Marubani wakiwa wanaelezea juu ya ndoto zao

  Walimu nao hawakuwa nyuma waliendelea na Burudani


  Baadhi ya wahitimu wa shule ya awali wakiwa katika sherehe yao
  Baadhi ya wanafunzi wanaobaki wakiwa katika mahafali hayo
  Wazazi wa watoto wanaosoma shule hiyo pamoja na wageni waalikwa wakiwa katika mahafali ya shule ya awali ya Brookhouse.Picha na Fredy Njeje wa Blogs za Mikoa
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: NAIBU WAZIRI WA ELIMU MH. MHANDISI STELLA MANYANYA AWA MGENI RASMI MAHAFALI YA BROOKHOUSE INTERNATIONAL SCHOOL JIJINI DAR Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top