728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, August 10, 2016

  NAIBU WAZIRI MPINA AIASA TAASISI YA MUUNGANO KUFANYA TAFITI ZENYE TIJA KWA SERIKALI NA UMMA.


  Kushoto Naibu Waziri Ofisi Ya Makamu wa Rais anaeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akipata Maelezo toka kwa Dkt. Mohammed Maalim Mtaalam wa Maabara ya Taasisi ya Sayansi za Bahari ya Chuo Kikuu cha DSM ..iliyopo Zanzibar, moja wapo ya taasisi ya Muungano ililopo chini ya Wizara ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Naibu Waziri Mpina Yupo Mjini Zanzibar katika ziara ya kikazi.
  Katika Picha ya pamoja aliyekaa kati kati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina pamoja na watumishi wa Taasisi ya ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, iliyopo Buyu katika wilaya ya Magharibi B nje kidogo ya mji mkongwe wa Zanzibar.
  Kushoto Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, kati kati ni Dkt. Yohana Shebule muhadhiri wa ya Taasisi ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, na Makamu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Profesa Mtolela wakitembea kukagua jengo jipya la taasisi hiyo lililopo Buyu, nje kidogo ya mji mkongwe wa Zanzibar.
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, pamoja na ujumbe wake wakisikiliza taarifa na changamoto za jengo jipya la za Taasisi ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, toka kwa dkt.Yohana Shebuda hayupo pichani, wakati wa kukagua jingo hilo pamoja na kuzungumza na watumishi wa taasisi hiyo
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina kushoto Pamoja na ujumbe wake.wakiendelea kukagua jengo la Taasisi ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi hiyo lililopo Buyu, nje kidogo ya mji mkongwe wa Zanzibar. (Picha na Habari zote na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais.) 
   

  Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anaeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. Luahaga Mpina Ametoa wito kwa taasisi za Muungano zinazofanya tafiti za kisayansi, kufanya tafiti hizo ziwe na tija kwa Serikali na Umma.

  Mpina aliyassema hayo, alipotembelea taasisi ya Muungano ya Sayansi za Bahari ya Chuo Kikuu cha DSM ..iliyopo katika Wilaya ya Magharibi B nje kidogo ya mji mkongwe wa Zanzibar, iliyopo chini ya Wizara ya Wizara ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Baada ya Kukagua jengo jipya la taasisi hilo ambalo halijaanza kutumika ikidaiwa ni kutokana na changamoto mbalimbali pamoja na ukosefu wa samani, Naibu Waziri Mpina aliishauri tafiti za taasisi hiyo ziwe zenye malengo ya kusaidia watanzia wanaoishi katika ukanda wa pwani ili kuwawezesha kusaidia kuinua uchumi wao na kuongeza pato la taifa.

  Aidha, Mpina aliongeza kwa kusema kuwa anategemea tafiti zinazofanywa na taasisi hiyo zitoe muongozo kwa serikali na namana ambavyo nchi inavyoweza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi. “Hakikisheni serikali inapata taarifa zenu ili ziweke kutumika, mpo kimya sana na hamsikiki.” Alisisitiza Mpina.

  Kwa upande mwingine taasisi hiyo imekuwa pia ikitoa nafasi kwa wanafunzi wageni toka katika nchi mbali mbali duniani kuja kujifunza na kufanya tafiti juu ya viumbe hai waishio baharini aina ya Pomboo (Dolphin)ili kuweza kufahamu mazingira na tabia za ndani za viumbe hao na kubadilishana uwezo na kuongeza kipato kwa taasisi hiyo kupitia malipo ya mafunzo hayo maalum. 
   
  Naibu Waziri Mpina pia, alitoa Pongezi kwa taasisi hiyo kuwa na jengo zuri pamoja na changamoto wanazokabilana nazo na kuwashauri wahamie na kuanza kulitumia jengo hilo. Ziara ya Naibu Waziri Mpina Mjini Zanzibar pamoja na kumuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano Mhe.Samia Suluhu Hassan katika siku ya Kizimkazi mkoa wa Kusini Unguja, inahusisha pia kutembelea baadhi ya taasisi za muungano mjini humo. 


  EVELYN MKOKOI

  AFISA HABARI

  OFISI YA MAKAMU WA RAIS

  HABARI KUTOKA ZANZIBAR 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: NAIBU WAZIRI MPINA AIASA TAASISI YA MUUNGANO KUFANYA TAFITI ZENYE TIJA KWA SERIKALI NA UMMA. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top