728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, August 11, 2016

  NAIBU KATIBU MKUU PROFESA JAMES MDOE ATEMBELEA MNADA WA TANZANITE JIJINI ARUSHA.

  Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini Profesa James Mdoe ametembelea mnada wa Madini ya Tanzanite yaliyochimbwa kutoka migodi ya Kampuni tano za wafanyabiasha wa madini hayo ili kuona utaratibu unaotumika kuwapata washindi wa zabuni za kununua madini ya hayo wakati wa mnada.

  Mnada huo unatarajia kufanyika Agosti 12 mwaka huu na unafanyia Tanzania kwa mara kwanza; Vilevile watakaoshinda zabuni za kununua madini ya hayo watatangazwa wakati wa mnada.Mnada huo umeshirikisha wafanyabiashara wa Madini wa ndani na nje ya Tanzania.

  Naibu Katibu Mkuu anayeshughulika Madini wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe ( kushoto) akionyeshwa namna ya kutambua ubora wa jiwe la Tanzanite na Mkurugenzi wa Uthaminishaji na Almasi na vito Tanzania( TANSORT) Archard Kalugendo( kulia).

  Naibu Katibu Mkuu anayeshughulika Madini wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe akitazama ubora wa jiwe la Tanzanite kupitia kifaa maalim.
  Naibu Katibu Mkuu anayeshughulika Madini wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe( kushoto )akizungumza na baadhi ya wauzaji wa Madini ya Tanzanite, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya VGL Group ,Sunil Agrawal( kulia), na Mmoja wa Wakurugezi wa Kampuni ya TanzaniaOne, Rizwan Ullah ( wa pili kulia) wakati wa mnada wa Madini ya Tanzanite mkoani Arusha.
  Naibu Katibu Mkuu anayeshughulika Madini wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe ( kushoto)akielezwa utaratibu wa kujaza fomu za kushiriki Mnada wa madini ya Tanzanite utakaofanyika Agosti 12 mkoani Arusha,kutoka kwa Mhandisi Juma Lunda( katikati) na Sekretari wa kituo cha Jimolojia Tanzania ( TGC)Halima Hussein(kulia) mnada huyo utafanyika Tanzania kwa mara.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: NAIBU KATIBU MKUU PROFESA JAMES MDOE ATEMBELEA MNADA WA TANZANITE JIJINI ARUSHA. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top