728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, August 29, 2016

  MWENYEKITI WA PAROLE AMEIOMBA SERIKALI KUTANUA HUDUMA YA METHADONE KWA WAHANGA WA DAWA ZA KULEVYA

  Mwenyekiti wa Bodi ya Parole, Agustino Mrema akizungumza na waandishi habari juu kuwasaidia wahanga wa dawa za kulevya leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi wa Msaidizi wa Idara habari MAELEZO, Vicent Tiganya
   
  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Mwenyekiti wa Bodi ya Parole, Agustino Mrema ameiomba serikali kuwasaidia wahanga wa dawa za kulevya ambao wako katika tiba kwa kuongeza huduma hiyo katika maeneo mbalimbali yenye wahanga hao

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mrema amesema kwa utafiti alioufanya baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam,amesema kuwa badala ya polisi kuwakamata wauzaji wadogo,wapaswa kuwakamata watu wakubwa wanaoleta na makontena na sio watu wenye kete mbili.

  Mrema ameiomba serikali kwa waliokuwa watumishi wa serikali walijingiza katika utumiaii wa dawa za kulevya hivyo warudishwe ili kuendelea na kazi.

  Amesema baadhi ya waliokuwa watumishi na wakajiingiza katika dawa za kulevya ni madereva, walimu pamoja Teknolojia ya mawasiliano (IT).

  Hata hivyo Mwenyekiti wa bodi ya Parole amesema wahanga wa dawa za kulevya wasaidiwe katika kuendesha maisha kutokana na kutumika na wanasiasa katika maandamano kwa kupewa kete za dawa za kuleva.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MWENYEKITI WA PAROLE AMEIOMBA SERIKALI KUTANUA HUDUMA YA METHADONE KWA WAHANGA WA DAWA ZA KULEVYA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top