728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, August 30, 2016

  MWANDISHI SIMON KIVAMWO ANAHITAJI DAMU KUOKOA MAISHA YAKE, SHIME WANAHABARI NA WADAU


  Bw. Simon Kivamwo
  Waandishi wa habari wakitoa damu ili kuwezesha matibabu ya Mwandishi wa habari mkongwe hapa nchini Bw. Simon Kivamwo ambaye anapatiwa matibabu kwenye hospitali ya Ocean Road iluyoko jijini Dar es Salaam leo Agosti 30, 2016. 
   
  Kwa mujibu wa Mwandishi wa Habari anayeratibu zoezi hilo Bw.Thompson, Kivamwo ambaye anaugua kwa muda mrefu sasa, amezidiwa na maradhi leo hii na kukimbizwa kwenye hospitali hiyo ambapo madaktari walihitaji kumuongezea damu. 
   
  Benjamin Thomspon ametoa wito kwa wanahabari na jamii kwa ujumla kujitokeza kumchangia damu mwanidhi mwenzetu ili kuokoa maisha yake. Sehemu ya kutolea damu ni Hospitali ya Mnazi Mmoja, Kariakoo jijini Dar es Salaam
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MWANDISHI SIMON KIVAMWO ANAHITAJI DAMU KUOKOA MAISHA YAKE, SHIME WANAHABARI NA WADAU Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top