728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, August 29, 2016

  MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI, MHE. GEORGE MASAJU AVIASA VYAMA VYA SIASA KUHESHIMU KATIBA YA NCHI

   
   Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG),George Masaju akifafanua masuala mbalimbali kuhusu wajibu wa Utii wa Sheria na kudumisha amani nchini,alipokuwa akizungumza mbele ya Wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar leo. 
   “Napenda kuvishauri vyama vya siasa nchini kuacha kutumia kauli za kibabe na vitisho kwa kisingizio cha kutumia haki zao za kikatiba, hali hiyo itapelekea vyombo vya dola kuchukua hatua kwani ni viashiria vya uvunjifu wa amani”. Amesema Mh.Masaju.
   Baadhi ya Wanahabari wakimsikiliza Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG),George Masaju alipokuwa akizungumza nao masuala mbalimbali yaliyohusu wajibu wa Utii wa Sheria na kudumisha amani nchini,alipokuwa akizungumza mbele ya Wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar leo.
    Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG),George Masaju akifafanua jambo alipokuwa akijibu maswali mbalimbali ya Waandishi wa Habari kuhusu wajibu wa Utii wa Sheria na kudumisha amani nchini,jijini Dar leo.
   Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG),George Masaju akifafanua masuala mbalimbali kuhusu wajibu wa Utii wa Sheria na kudumisha amani nchini,alipokuwa akizungumza mbele ya Wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar leo.PICHA NA MICHUZI JR

  Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar leo,Masaju amesema kuwa polisi wamesema kuwa wana hali ya kuzuia mikutano na maandamano iwapo watabaini kuwa yataibuka mambo yatakayohatarisha amani ya nchi,Masaju amesema kuwa maandamano hayo yataleta madhara na athari kama maandamano hayo ya UKUTA-Septemba mosi mwaka huu.

  Amesema kuwa madhara na athari ya maandamano hayo ni kubwa kutokana na siku hiyo itakuwa mahsusi kwa ajili ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ ikiwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwao,akaonngeza kuwa siku hiyo kutakuwa na tukio muhimu la kupatwa kwa Jua huko Lujewa mkoani Mbeya ambapo ni muhimu kwa nchi kupata manufaa kwa Watalii kuja kwa wingi na kuweza kunufaika Kiuchumi. 

  Masaju amesema kuwa vyama vya siasa nchini vinatakiwa kutumia vyema haki zao za msingi zilizoanishwa katika katiba badala ya kutumia, nguvu, ubabe na kupelekea kutishia hali ya amani na utulivu iliyopo nchini.

  Masaju amesema kuwa kumekuwa na baadhi ya wanasiasa wanaotoa vitisho vya kuitisha mikutano kinyume na taratibu za kisheria kwa kisingizio cha haki za kikatiba jambo ambalo sio kweli.“Napenda kuvishauri vyama vya siasa nchini kuacha kutumia kauli za kibabe na vitisho kwa kisingizio cha kutumia haki zao za kikatiba, hali hiyo itapelekea vyombo vya dola kuchukua hatua kwani ni viashiria vya uvunjifu wa amani”.

  Masaju aliwataka Wanasiasa kuwa wakweli na kuacha kuwapotosha wananchi kuwa wananyimwa haki ya kufanya mikutano kwani wapo baadhi yao wanaofanya mikutano katika majimbo yao baada ya Jeshi la Polisi kujidhirisha kwamba kutakuwa na hali ya amani na utulivu”. Alisema Mhe. Masaju.

  Aidha Masaju alipongeza juhudi zinazofanywa na viongozi mbalimbali wa dini nchini kwa jitihada wanazofanya za kushauri katika kufika muafaka wa hali ya kisiasa nchini na kuwashauri kuhubiri amani na utulivu kwa waumini wao. 

  Akitoa ufafanuzi wa tamko la baadhi ya vyama vya upinzani kutaka serikali kuvifuta vyama hivyo Mhe. Masaju alisema kuwa suala hilo ni kinyume na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu katiba hiyo inaruhusu mfumo wa vyama vingi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI, MHE. GEORGE MASAJU AVIASA VYAMA VYA SIASA KUHESHIMU KATIBA YA NCHI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top