JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MWAKILISHI WA JIMBO LA MAHONDA, BALOZI SEIF ALI IDDI AANZA KUTEKELEZA AHADI ZAKI.

Share This
 Msimamizi wa Ujenzi wa jengo la Maabara la Skuli ya Sekondari ya Fujoni Nd. Yasir De Costa wa pili kutoka kushoto akimpatia maelezo Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif  hatua iliyofikia ya ujenzi wa jengo hilo wakati alipofanya ziara ya kulikagua jengo hilo.
 Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi akijiandaa kumkabidhi vifaa vya Maabara ya Skuli ya Sekondari ya Fujoni Mwalimu wa Somo la Biology Mwalimu Khalid Hamad Khamis aliyevaa kofia ya kiua akitekeleza ahadi aliyotoa wakatiwa Kampeni za Uchaguzi Mkuu Oktoba Mwaka uliopita.
Picha na – OMPR – ZNZ.
                                 
Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba kazi ya utekelezaji wa ahadi aliyotoa kwa Wananchi wa Jimbo hilo wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka uliopita itaendelea hatua baada ya hatua ili kukidhi matarajio yao.

Alisema utekelezaji huo una dhamira ya kuwaondoshea kiu waliyonayo Wananchi hao katika kutatua kero pamoja na changamoto mbali mbali zinazowakabili katika maeneo yao wanayoishi.

Balozi Seif alisema hayo wakati akibabidhi vifaa vya Maabara kwa Skuli ya Sekondari ya Fujoni akitekeleza ahadi aliyowapa Wanafunzi, Walimu na Uongozi wa Kamati ya Skuli hiyo vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi Milioni  25,000,000/- za Kitanzania.

Alisema wakati Viongozi na Kamati ya Skuli wakijitahidi kujenga mazingira bora ya Kielimu kazi inayowakabili wanafunzi hao kwa sasa ni kuhakikisha wanajikita zaidi katika kutafuta Elimu kwa lengo la kujijengea hatma njema ya maisha yao ya baadaye.

Mapema Balozi Seif Ali Iddi alipata wasaa wa kukagua Jengo jipya la Maabara aliloligharamia ujenzi wake katika Skuli hiyo ya Fujoni ambalo limefikia hatua nzuri katika kukamilika kwake.

Msimamizi wa Ujenzi wa Jengo hilo Ndugu Yasir De Costa alimueleza Balozi Seif kwamba ujenzi wake umeshakamilika kwa hatua ya awali ikiwemo uwepo wa huduma ya Maji na kilichosaliwa kwa wakati huu ni umakilishaji wa huduma za Umme kwa ajili ya kutumiwa na wanafunzi hao.

Ujenzi wa jengo hilo Jipya la Maabara la Skuli ya Sekondari ya Fujoni unakisiwa kugharimu zaidi ya shilingi Milioni 30,000,000/-.

Fujoni ni miongoni mwa Skuli Tatu za Sekondari  zilizomo ndani ya Jimbo la Mahonda mbayo kutokana na juhudi za Walimu na Kamati ya Skuli tayari imebahatika kuwa na Darasa la Kumi na Nne { Form VI }.
Othman Khamis Ame

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
1/8/2016.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad