728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, August 18, 2016

  Muhimbili Yafanya Upasuaji kwa Watoto Wenye Tatizo Mfumo wa Hewa na Njia ya Mkojo

  Kutoka kulia ni Dk. Zaitun Bokhary na Dk. Yona Ringo wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wakimfanyia upasuaji mtoto mwenye tatizo kwenye mfumo wa hewa na chakula LEO kwa kushirikiana na Profesa Saber M. Waheeb (kushoto) na wenzake kutoka Misri.
  Kutoka kulia ni Dk. Yona Ringo na Dk. Zaitun Bokhary wa Muhimbili wakiendelea na upasuaji kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Misri.
  Profesa Saber M. Waheeb (katikati) akijadiliana jambo na Dk. Zaitun Bokhary kabla ya kuanza kwa shughuli ya upasuaji kwa watoto wanane LEO. Kutoka kushoto ni Mwambata wa Jeshi la Wananchi Tanzania, Kanali Salum Haji Othman nchini Misri na nchi zote za Mashariki ya kati na Dk Yona Ringo wakifuatilia mazungumzo hayo LEO.
  Grace Joel akiwa na watoto wake pacha, Eliudi Joel (katikati) na Elikana Joel wakisubiri kufanyiwa upasuaji wad njia ya mkono. Awali watoto hao kutoka Mbeya walizaliwa wakiwa wameungana na baadaye walifanyiwa upasuaji na kutenganishwa.
  Kutoka kushoto ni Eliudi Joel na Elikana Joel wakiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wakisubiri kufanyiwa upasuaji LEO.
  Profesa Dk. Saber M. Waheeb akifanya utafiti mdogo kwa mtoto ambaye amelazwa kwenye Jengo la watoto katika hospitali hiyo.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru (kushoto) akimkaribisha Profesa Saber M. Waheeb katika hospitali hiyo LEO.
  Profesa Lawrence Museru (kulia) akizungumza na madaktari na wataalamu wa kada nyingine LEO katika hospitali hiyo kabla ya kuanza kwa shughuli ya upasuaji.
  Kutoka kushoto ni Mwambata wa Jeshi la Wananchi Tanzania, Kanali Salum Haji Othman nchini Misri na nchi za Mashariki ya kati akizungumza jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji, Dk. Julieth Magandi LEO wa hospitali hiyo.
  ……..
  Na John Stephen 

  Dar es Salaam, Tanzania. Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) LEO imeanza upasuaji kwa watoto wanane na wenye matatizo ya njia ya mkojo na mfumo wa hewa na chakula ili kuwa sawa na watu wengine ambao hawana matatizo hayo. 

  Madaktari wa hospitali hiyo wanafanya upasuaji huo kwa kushirikiana na madaktari kutoka Misri ambao wamewasili leo wakitokea Misri kwa ajili ya kushiriki shughuli hiyo. 

  Madaktari wa Muhimbili ni Dk. Zaitun Bokhary, Dk. Yona Ringo Madaktari, Dk. Herman Wella, Dk. Victor Ngolta, Dk Mwajabu Mbaga, Dk. Joachim Angela, Dk. Hashim Lituli na Dk. Gertrud Mollel wakati madaktari na wataalamu wa kada nyingine kutoka Misri ni Mahamed Malak, Saber Waheeb, Amr Alaa, Tamer Ghoneim, Ragia Mohamed Awad, Sherouk Saad Ayoub, Hazem Ahmed. 

  Wataalamu hao wametembelea watoto waliolazwa kwenye Jengo la Watoto na kujadiliana na madaktari wa hospitali hiyo jinsi watakavyotoa huduma za upasuaji kwa watoto hao.
  Kwa mujibu wa Dk Julieth Magandi, watoto wengine sita watafanyiwa upasuaji huo kesho. Dk Magandi amesema Leo madaktari hao wameanza kwa mtoto mwenye tatizo la mfumo wa chakula na hewa na kwamba watoto pacha wawili waliungana na kutenganishwa kutoka Mbeya nao watafanyiwa upasuaji wa kuweka sawa mfumo wa njia ya mkojo. 

  Baadhi ya watoto wanaofanyiwa upasuaji ni; Nasra Rashidi, Hughes Khalid, Fahad Selemani, Elikana Joel, Eliudi Joel, Hasna Hamis Kalemea, Ibrahim Haji na Sofia Ramadhani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Muhimbili Yafanya Upasuaji kwa Watoto Wenye Tatizo Mfumo wa Hewa na Njia ya Mkojo Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top