728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, August 26, 2016

  MSHINDI WA TUZO NA MWANAMUZIKI MACHACHARI KUTOKA NCHINI NIGERIA 'YCEE ' KUKONGA NYOYO ZA WATANZANIA KATIKA ZIARA YAKE BARANI AFRIKA

  YCEE ambaye pia hufahamika kwa jina la Oludemilade Martin Alejo, anatarajiwa kufika jijini Dar es salaam tarehe 28th Agosti 2016 , ikiwa ni sehemu ya ziara yake yenye lengo la kutangaza nyimbo zake ambazo ni Omo Alhaji, Jagabana' na nyinginezo.

  Ziara hiyo itaambatana na mkutano wa waandishi wa habari siku ya Jumatatu tarehe 29th Agosti 2016, ikifuatiwa na ziara ya kutembelea vituo mbalimbali vya habari kuanzia tarehe 29th Agosti 2016 mpaka tarehe 1 Septemba 2016.

  Msanii huyo aliyepata umaarufu kupitia wimbo wa ' Jagaban ' na ' Omo Alhaji ' amedhamiria kuungana na mashabiki, wazalishaji wa muziki na wasanii mbalimbali hapa nchini ili waweze kujenga mahusiano imara zaidi.

  Pamoja na hayo amesema kuwa, anayo shahuku kubwa juu ya ziara yake kwani hii ni mara yake ya kwanza hapa nchini."Nina hamu sana ya kukutana na mashabiki wangu wa Tanzania, kwa sababu upendo wanaonipa kupitia mitandao ya kijamii ni wa ajabu na nina furaha sana ya kukutana na watu wapya " , alisema.

  Baada ya ziara yake nchini Tanzania , YCEE ataenda nchini South Africa kuendelea na ziara yake yakukuza na kutangaza muziki wake, na anatarajia kuachia orodha ya nyimbo mpya baadaye mwaka huu utakao fahamika kwa jina la ‘The First Wave'. Msanii huyo wa Omo Alhaji 'YCEE' pia ni miongoni mwa wasanii wanaopenda kusaidia jamii kwa kuwafikia vijana wa kiafrika katika masuala ya maendeleo na michezo.

  Hivyo katika ziara yake hapa nchini YCEE atatoa msaada wa fedha kwa kituo cha masuala ya umaskini na ukosefu wa upatikanaji wa elimu kwa watoto wa mitaani Kigamboni. Kigamboni Community Center (KCC) , ni kituo kinacho shughulika na masuala ya kutokomeza umaskini, huku kikijikita katika kutoa elimu ya chekechea na msingi kwa watoto ambao wako mbali na upatikanaji wa elimu. 
   
  KCC pia hutoa fursa nyingine za kujifunza kwa vijana wa Kigamboni, na pia hutoa elimu ya jamii, madarasa ya kuendeleza vipaji na mafunzo ya ufundi stadi. YCEE ameamua kuunga mkono kituo hiki kwa kwa sababu ya kujitolea kwao kukuza vipaji na kujenga upatikanaji wa elimu kwa jamii.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MSHINDI WA TUZO NA MWANAMUZIKI MACHACHARI KUTOKA NCHINI NIGERIA 'YCEE ' KUKONGA NYOYO ZA WATANZANIA KATIKA ZIARA YAKE BARANI AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top