728x90 AdSpace






 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, August 31, 2016

  MNEC MUFINDI AWATAKA WANANCHI KUJIANDAA NA MILIONI 50 ZA RAIS DR MAGUFULI .


  Na MatukiodaimaBlog

  WANANCHI wilayani Mufindi mkoani Iringa wametakiwa kuanza maandalizi ya kunufaika na milioni 50 kwa kila kijiji zilizopangwa kutolewa na Rais Dr John Magufuli kwa kuanza kujiunga vikundi vya ujasiriamali na kuvisajili .

  Wito huo umetolewa na mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha mapinduzi (CCM) Taifa kutoka wilaya ya Mufindi ,Marcelina Mkini wakati akizungumza na wanahabari kuhusu utaratibu huo mzuri ulioahidiwa na Rais Dr Magufuli wakati wa kampeni .

  Alisema kuwa ili wananchi kuweza kunufaika na utaratibu huo ni lazima kujiunga katika vikundi vya watu wenye malengo yanayofanana na kuvisajili ili pindi pesa hizo zitakapotolewa kuweza kuzipata .

  Mkini alisema kwa utaratibu wa fedha hizo hazitatolewa kwa mtu mmoja mmoja hivyo kwa wale ambao wanazitamani fedha hizo ni lazima kuanza kujiunga katika vikundi ambavyo vimesajiliwa .

  " Lengo la Rais wetu ni kuona wananchi wananufaika na matunda ya nchi hii ndio sababu ya kuahidi kusaidia vijiji fedha hizo shilingi milioni 50 kwa kila kijiji fedha ambazo ni nyingi sana na zitasaidia wananchi kujikwamua katika dimbwi la umasikini lazima tumpongeze sana kwa mtazamo huu ambao haujapata kutokea ".

  Hivyo alitaka vijana ,wanawake na wazee kujiunga makundi yenye malengo yanayofafa yakiwemo ya ufugaji kwa wazee ama kilimo na makundi mengine ambayo yatapelekea vijiji kuwa na vyama vya kuweka na kukopa (SACCOS) zao .

  Mkini ambae pia ni mwenyekiti wa umoja wa wanawake Tanzania (CWT) wilaya hiyo ya Mufindi aliwataka viongozi wote wa UWT ngazi zote kusaidia kuhamasisha wanawake kuonyesha mfano katika kuanzisha vikundi vya uzalishaji mali .

  Huku akiwataka kwa kipindi hiki cha kuelekea kupata fedha hizo kuwa makini na matapeli ambao baadhi ya mikoa wameanza kujipitisha kudanganya wananchi kuwa fedha hizo zitapitia katika NGOs zao .
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MNEC MUFINDI AWATAKA WANANCHI KUJIANDAA NA MILIONI 50 ZA RAIS DR MAGUFULI . Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top