728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, August 9, 2016

  MHE. KAIRUKI AWATAKA WATUMISHI WA OFISI YAKE KUWA MFANO KATIKA KUTOA HUDUMA BORA


  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati) akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi cha robo mwaka cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) na watumishi wa ofisi yake kilichofanyika Utumishi leo. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Aloyce Msigwa.
  Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha robo mwaka cha waziri huyo na watumishi wa ofisi yake kilichofanyika Utumishi leo.
  Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Aloyce Msigwa (kushoto) akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi wakati wa kikao kazi cha robo mwaka cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (kulia) na watumishi wa ofisi yake kilichofanyika Utumishi leo.Katikati ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro akisikiliza kwa makini.
  Mtumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Victor Kitu (aliyesimama) akiwasilisha malalalamiko yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha robo mwaka cha waziri huyo na watumishi wa ofisi yake kilichofanyika Utumishi leo.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa ofisi yake wakati wa kikao kazi cha robo mwaka cha waziri huyo na watumishi wa ofisi yake kilichofanyika Utumishi leo. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Utumishi Bw. Kamugisha Rufulenge.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (MB.) amewataka Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kutoa huduma bora kwa wadau ili kujenga taswira nzuri ya Ofisi hiyo.

  Mhe. Kairuki aliyasema hayo wakati wa kikao kazi cha robo mwaka na watumishi wa Ofisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.

  Alisema, Ofisi ya Rais – Utumishi kama jina lenyewe lilivyo, inatakiwa kuwa kioo na mfano wa kuigwa na taasisi nyingine za Serikali kwa kutoa huduma bora na kwa wakati kwa wadau wake. he. Kairuki aliwataka watumishi hao kuangalia ni kwa jinsi gani huduma wanazotoa kwa wadau zinazingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo katika utumishi wa umma.

  “Tutoe huduma kwa kuzingatia taratibu zilizopo na uadilifu mkubwa,” Mhe. Kairuki alisisitiza. Aliongeza kuwa, wapo baadhi ya watumishi wana majibu ya hovyo sana kwa wateja, hivyo aliahidi kuwafuatilia, na iwapo wakibainika hatua stahiki za kinidhamu zitachukuliwa dhidhi yao.

  Aidha, Mhe. Kairuki aliwataka watumishi hao kuwa na utamaduni wa kujisomea na kufanya tafiti mbalimbali katika maeneo wanayoyafanyia kazi ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi. “Wapo baadhi ya watumishi hawana utamaduni wa kujisomea, wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea na matokeo yake hujikuta wakishindwa kufanya inavyopaswa.” Mhe. Kairuki alisisitiza.

  Mhe. Kairuki amejiwekea utaratibu wa kukutana na watumishi wa ofisi yake kila robo mwaka kwa lengo la kuzungumzia masuala mbalimbali ya kiutumishi na kiutendaji.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MHE. KAIRUKI AWATAKA WATUMISHI WA OFISI YAKE KUWA MFANO KATIKA KUTOA HUDUMA BORA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top