728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Saturday, August 13, 2016

  MBUNGE ULEGA AWATAKA WANANCHI WA KIJIJI CHA MWALUSEMBE KUILINDA MIUNDOMBINU YA KISIMA IKIWAMO SOLAR  Mbunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwalusembe kweye hafla ya uziduzi wa kisima cha Maji katika kijiji cha Mwalusembe, ambacho kimejengwa katika shule ya msingi Muongozo kwa ufadhili wa Taasisi ya Afraca Reflection Foundation leo mkoani Pwani.
  .Mbunge wa jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akizindua kisima cha Maji katika kijiji cha Mwalusembe ambacho kimejengwa katika shule ya msingi muongozo Kwa ufadhili wa Taasisi ya Afraca Reflection Foundation leo mkoani Pwani.

  Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akiwasil katika kijiji cha Mwalusembe kwa ajili ya kuziduzi kisima cha Maji ambacho kimejengwa katika shule ya msingi Muongozo mkoani Mpwani.
  (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)

  Mbunge wa jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega amezindua kisima cha Maji katika kijiji cha Mwalusembe ,ambacho kimejengwa katika shule ya msingi muongozo Kwa ufadhili wa Taasisi ya Afraca Reflection Foundation
  Mara baada ya uzinduzi huo,Mh. Ulega aliwashukuru wafadhili hao na kuwaomba kuendelea kusaidia wilaya hiyo ili kukabiliana na uhaba wa Maji uliopo na kuwa Wilaya ya Mkuranga ni moja ya maeneo ambayo yanachangamoto kubwa ya Maji.
  Mh.Ulega Pia aliwataka wananchi wa kijiji hicho kutumia Maji hayo vizuri ikiwa pamoja na kulinda miundombinu yake ikiwamo solar na vinginevyo ili visiibiwe,Mh Ulega tangu kuchaguliwa kwake kuwa Mbunge wa jimbo hilo tayari ameshachimba visima katika vijiji zaidi ya vitano huku akisaidia kutatua mbalimbali ya wananchi ambayo yamekuwa kero kwao
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  1 comments:

  1. Hapo ndipo wapinzani wanapo kereketwa wao wameweka mbele kuandamana tu hiyo tarehe 1/9/16
   Waandamane wakione hatujaribiwi tia mguu rodi watu tunavunja shingo
   CCM oye

   ReplyDelete

  Item Reviewed: MBUNGE ULEGA AWATAKA WANANCHI WA KIJIJI CHA MWALUSEMBE KUILINDA MIUNDOMBINU YA KISIMA IKIWAMO SOLAR Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top