728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, August 16, 2016

  MBUNGE ULEGA ASHIRIKI KUHAMASISHA WANANCHI KUFYATUA MATOFALI KWA AJILI YA UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI


   Mbunge wa Jimbo la mkuranga Abdallah Ulega akishiriki kufyatua tofari za  ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kikundi kilichopo kata ya Mkamba wilayani Mkuranga,mbali na kushiriki huko pia alichangia viloba vya unga wa sembe,maharagwe,maji ya kunywa kutokana na vijana wa kijiji hicho kuweka kambi ya kufyatua matofali hay oleo mkoani Mpwni.
   Wazee wa kijiji cha Kikundi ,kilichopo kata ya Mkamba wilayani mkuranga  wakiteta jambo na mbunge wa jimbo hilo Abdallah ulega, ambapo pamoja na mambo mengine walimpongeza mbunge huyo kwa kuonesha moyo wa kuitumikia wilaya hiyo nakudai katika wabunge saba waliotangulia haijawahi kutokea katika kile anachofanya Ulega ikiwamo kufanya ziara za vijiji kwa lengo lakuwashukuru.
  Vijana wa kijiji cha kikundi ,kata ya mkamba wakiwajibika katika kufyatua matofali ya ujenzi wa Zahanati kijijini hapo ambapo kwa muda mrefu imekuwa kero kubwa hali inayowafanya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo katika kijiji cha kizapala wilayani humo.
  (Pichs na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)

  Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega ameshiriki na kuhamasisha wananchi wa Kijjji cha kikundi ,kata ya mkamba kufyatua matofali Kwa ajili ya Ujenzi wa Zahanati ya kijiji hicho. 

  Akiwa katika eneo la tukio alishirikiana kikamilifu na vijana ,wazee ,na akina mama waliojitokeza Kwa wingi Kwa ajili ya kujitolea,akizungumza katika eneo hilo akiwa sambamba na Diwani wa Kata hiyo Hassan Dunda, mbunge Ulega aliwaeleza wananchi hao kuwa ameshiriki shughuli hiyo ikiwa sehemu ya majukumu yake na ahadi alizotoa Kwa watu wake na kwamba maendeleo ya kijiji cha kikundi na Mkuranga Kwa ujumla yataletwa na wao wenyewe. 

  Alisema kuwa katika kipindi chake chote cha ubunge atahakikisha anafanya mambo makubwa Kwa ajili ya maendeleo ya wilaya hiyo huku akidai kuwa Mkuranga imechelewa sana lazima wakimbie mbio. Kwa upande wa Wazee wa kijjji hicho wamesema kuwa Ulega ameonesha nia ya dhati mno katika uongozi wake na wanaimani naye sana kwamba atafanya mambo mengi makubwa. 

  Akizungumza kwa niaba ya Wazee wezake Idrisa Pelete amesema kuwa kuna wabunge wengi wamepita na hawakuweza kufanya lolote lakini Kwa sasa wanaamini wamepata kiongozi wa kweli na hicho ndicho walikuwa wanakihitaji.Pia Kijana aliyejitambulisha kuwa ni shaweji Mohammed akitoa neno la shukrani Kwa mbunge alisema kuwa pamoja na kwamba yeye ni mpinzani lakini kwa kazi kubwa alionesha Mbunge kwakweli wanampenda mno.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MBUNGE ULEGA ASHIRIKI KUHAMASISHA WANANCHI KUFYATUA MATOFALI KWA AJILI YA UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top