728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, August 17, 2016

  Mafunzo ya Menejimenti ya Tume ya Taifa ya uchaguzi kuhusu Vihatarishi vya malengo kufanyika kwa siku tano.  Na Clarence Nanyaro,Morogoro

  Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeanza mafunzo ya siku tano kuhusu namna ya kutambua vihatarishi vya utekelezaji wa malengo na jinsi ya kukabiliana navyo.

  Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika mjini Morogoro kwa niaba ya Mkurugenzi wa uchaguzi,Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bwana Salvisius Nkwera amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa Watendaji na Watumishi wa Tume ili kufahamu vihatarishi ambavyo vinaweza kukwamisha utekelezaji wa malengo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatekeleza jukumu la kuwa na daftari la vihatarishi vya malengo,kwa mujibu wa sera ya Serikali ambayo inataka kila Taasisi kuwa na daftari la viatarishi vya malengo ili kuziwezesha taasisi hizo kufikia malengo au kubainisha namna ya kukabiliana na vihatarishi hivyo.

  Wanaoshiriki katika mafunzo hayo ni Wakuu wa Idara na Vitengo toka Tume ya Taiafa ya Uchaguzi na mabao kabla ya kumalizika kwa mafunzo hayo watatengeneza rasimu ya daftari la vihatarishi vya malengo kwa ajili ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

  Naye Mkufunzi wa mafunzo hayo toka Kampuni ya Posta nchini,Bwana Macrice daniel Mbodo,amesema sheria inaelekeza kuwa kila Taasisi hapa nchini kuwa na daftari la vihatarishi vya malengo ili kurahisisha ukaguzi wa utekelezaji wa malengo ya Taasisi husika.

  Bwana Mbodo amesema kuwa,uwepo wa daftari la hilo la vihatarishi vya malengo,kayika kila Taasisi ni kwa mujibu wa sheria na utekelezaji wake unafuata taratibu za Kimataifa.

  Sambamba na mafunzo hayo,Menejimenti pia itaandaa Mwongozo wa manunuzi na Lojistiki kwa ajili ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi,mwongozo ambao utasaidia washisani mbalimbali wanaotaka kufanya kazi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi

  Mafuznzo hayo a,mbayo yatakamilika Ijumaa 19.08.2016,yatawasaidia Watendaji wa Tume ya Taifa ya uchaguzi kupata rasimu ya Fdaftari la vihatarishi vya Malengo na kufanya rejea kujlingana na mabadiliko ya Wakati.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Mafunzo ya Menejimenti ya Tume ya Taifa ya uchaguzi kuhusu Vihatarishi vya malengo kufanyika kwa siku tano. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top