728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, August 11, 2016

  MAFUNDI TEMESA WAPIGWA MSASA


  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. William Nshama (mwenye koti jeusi) akisikiliza maelezo kuhusu namna kifaa cha kukagua taa za magari kutoka kwa mmoja wa mafundi wa Kituo cha Ukaguzi wa Magari cha Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa mafunzo ya siku 14 kwa mafundi wa TEMESA hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.Picha zote na Frank Shija, MAELEZO.


  Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Dkt. Mhandisi Prosper Mgaya akifafanua jambo mara baada ya kumpokea Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. William Nshama(aliyevaa tai) alipowasili Chuo hapo kwa ajili ya uzinduzi wa mafunzo ya siku 14 kwa mafundi 25 wa TEMESA yanayoendelea Jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo mafundi hao katika Nyanja za matumizi ya vifaa vya kisasa, utambuzi wa vilainishi halisi, na ubora wa matairi. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Ufundi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Vazuri Lazaro Mbise.
  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. William Nshama akielezea jambo wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya siku 14 kwa mafundi wa TEMESA hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo mafundi hao katika Nyanja za matumizi ya vifaa vya kisasa, utambuzi wa vilainishi halisi, na ubora wa matairi ambapo jumla ya mafundi 25 wanashiriki. Kutoka kulia ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Dkt. Mhandisi Prosper Mgaya, Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo kutoka TEMESA Mhandisi. Sylivester Semfukwe na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Ufundi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Vazuri Lazaro Mbise.
  Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TEMESA Mhandisi Le Kujan Manase akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya siku 14 kwa mafundi wa TEMESA hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. William Nshama.
  Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Dkt. Mhandisi Prosper Mgaya akielezea jambo wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya siku 14 kwa mafundi wa TEMESA hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TEMESA Mhandisi Le Kujan Manase, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. William Nshama, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Ufundi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi, Vazuri Lazaro Mbise na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo kutoka TEMESA Mhandisi. Sylivester Semfukwe.
  Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya ufundi kutoka TEMESA na wadau wa mafunzo hayo wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mafunzo hayo iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) hivi karibuni.

  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. William Nshama (watatu mwenye tai) akiangalia hatua za ukaguzi wa gari katika Kituo cha Ukaguzi wa Magari kilichopo Chuo cha Cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) hivi karibuni wakati wa hafla uzinduzi wa mafunzo ya siku 14 kwa mafundi wa TEMESA hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Wapili kutoka kushoto ni Meneja wa Kituo hicho Mhandisi. Hans Mwaipopo.
  Na: 
  Frank Shija, MAELEZO

  Mafundi wa TEMESA watakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia weledi katika kutekeleza majukumu yao ili kupunguza malalamiko ya wateja wao.

  Hayo yamebainishwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. William Nshama wakati akifungua mafunzo ya mafundi hao hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.

  Dkt. Nshama aliosema kuwa mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka kwani yataongeza ufanisi kwa mafundi wa Serikali hivyo kuongoa malalamiko ambayo yamekuwapo kuwa TEMESA imekuwa ikifanya kazi za matengenezo ya magari na mitambo chini ya kiwango.

  “Kupitia mafunzo haya ni matumaini yangu kuwa mafundi wa TEMESA watakuwa na uwezo mkubwa wa kufanya kazi zao kwa weledi ikiwemo uwezo wa kutumia vifaa vya kisasa katika kutambua vipuli halisi na feki, na kubaini mchanganuo wa gharama halisi za matengenezo ya magari ili kuondoa malalamiko ya mara kwa mara”. Alisema Dkt. Nshama.

  Kwa upande wake Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TEMESA Mhandisi Le Kujan Manase amesema kuwa kutokana na mafunzo hayo kushirikisha mafundi 25 kutoka karakana mbalimbali zilizo chini ya TEMESA ni dhahiri kuwa zitaongeza ufanisi katika kutoa huduma ya ufundi kwa wateja ambao kwa kiasi kikubwa ni magari na mitambo inayomilikiwa na Serikali pamoja na taasisi zake.

  “Hapa kuna jumla ya mafundi 25 maana yake ni kwamba kila karakana nchini ina wataalam waliopata mafunzo ya kutumia vifaa vya kisasi, mkishirikiana kazi zenu zitakuwa na tija”. Alisema Mhandisi Manase.

  Naye Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Dkt.Mhandisi Prosper Mgaya amesema kuwa Chuo chake kitanendelea na jitahada za kuhakikisha kinaendesha program mbalimbali kwa lengo la kuboresha sekta ya usafirishaji nchini ikiwemo kuandaa mafundi kwa ajili ya vyombo vya usafiri wa aina mbalimbali.

  Mafunzo haya ya mafundi wa TEMESA yanafanyika kwa ushirikiano baina ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT),Kampuni ya Superdoll Trailer na TEMESA yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo mafundi katika Nyanja za matumizi ya vifaa vya kisasa, utambuzi wa vilainishi, ubora wa matairi na ukaguzi wa magari.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MAFUNDI TEMESA WAPIGWA MSASA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top