728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Wednesday, August 3, 2016

  KITUO CHA WATOTO WACHANGA YATIMA NJOMBE CHAOMBA MSAADA WA MASHINE YA KUFULIA.

  Baadhi ya wafanyakazi wa kituo cha kulelea watoto wachanga Yatima na lishe cha kipengere Mkoani Njombe wakifua nguo za watoto kwa mikono baada ya mashine walizokuwa wakizitumia kuharibika, Picha na James Festo.

  Na James Festo, Njombe.

  KITUO cha kulelea watoto yatima na lishe cha Kipengere kinachopatikana wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe ambacho huwahumia watoto wachanga yatima wenye umri wa miaka 0 hadi mitano kimewaomba wadau kusaidia kununua na kutengeneza mashine ya kufulia kutokana na zilizokuwapo kuharibika baada ya kutumika muda mrefu.

  Msimamizi wa kituo hicho ambacho kwa sasa kinawahudumia watoto 51 miongoni mwa 220 ambao waliwahi kuhudumiwa na kituo hicho, Sister Nivardina Mbifile aliliambia gazeti hili mwishoni mwa juma kwamba kwa sasa hulazimika kuamka saa kumi na moja asubuhi kufua nguo za watoto tofauti na hapo kabla.

  ""tunachangamoto kubwa sana ya mashine ya kufulia, tulikuwa nazo zimezeeka zimeharibika sasa tunafua nguo kwa mikono sasa watoto ni wengi tunaamka saa 10 kufua nguo za watoto hadi jioni tulionao ni wachanga ...hapo mwanzo tulikuwa na mashine hata wafuaji walikuwa wanapata nafuu...sasa hivi mikono inachubuka kwa sasa" alisema Sister Mbifile.

  Aliongeza kuwa "mashine hizi mbili zilishawahi kusumbua na tulisubiri wataalamu kutoka nje ya nchi wakaja kututengenezea zikaendelea kufanya kazi na sasa hatuwezi kutengeneza tena...na hii moja haina mda mrefu tumeacha kuitumia kwa sababu ilianza kuleta maneno ya kichina hivyo tunasubiri wataalamu kutoka nje wakiwahi watakuwa wametusaidia sana ila tunaomba mwenye uwezo wa kutusaidia atusaidie.

  Umoja wa wananchi wa Njombe Magharibi waishio jijini Dar es salaam UWENDE ni miongoni mwa waliofika kutoa msaada ya vyakula na mahitaji muhimu kwa watoto yatima katika kituo hicho wakiongozwa na Pascal Ngilangwa wenye thamani ya shilingi milioni 1.08 wakizungumza baada ya kuzungumza na wafuaji wa Nguo za watoto ambao wengi ni wachanga walisema msaada wa mapema unahitajika.

  "kufua kwa mkono nguo za watoto ambao baada ya saa moja huwa hazitazamiki kama nepi ni jambo linalohitaji moyo tena si kidogo tunaomba wadau wengine wasaidie kupatikana kwa mashine ya kufulia... hata viongozi wa serikali wasaidie hadi Rais wangu Magufuli mimi namlilia aje asaidie kutengeneza mashine au kununua mashine ya kufulia" alisema Ngilangwa.

  Aliongeza kuwa "sisi tumeamua kujitolea msaada ni jadi yetu tumekuwa tukisaidia kwenye upande wa elimu, kilimo, afya na mazingira sisi huchangishana na kutoa misaada hii kila mwaka katika maeneo mbalimbali.

  Kulingana na Sister Mbifile sehemu kubwa ya watoto ambao hulelewa kituoni hapo wamewapoteza wazazi wao kutokana na ugonjwa wa ukimwi pamoja na matatizo ya uzazi wakati wanapojifungua na asilimia kubwa ni kutoka wilaya za Makete, Njombe na Wanging'ombe. Itakumbukwa Mkoa wa Njombe kwa sasa ndio unaongoza kwa kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ya virusi vya Ukimwi kinachofikia asilimia 14.8 kulingana na utafiti wa Tume ya kudhibiti ugonjwa wa Ukimwi humu Nchini TACAIDS iliyotolewa mwanzoni mwa muongo wa pili wa karne ya 21
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: KITUO CHA WATOTO WACHANGA YATIMA NJOMBE CHAOMBA MSAADA WA MASHINE YA KUFULIA. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top