728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, August 16, 2016

  KAMISHNA WA TRA AZINDUA KAMPENI YA KUHAKIKI NAMBA YA MLIPA KODI (TIN)

  Kamishna wa TRA Bw. Alphayo Kidata akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TRA jengo la Milenium Makumbusho leo wakati akielezea kampeni ya kuhakiki namba ya utambulisho wa mlipa kodi TIN itakayoendelea mpaka mwezi wa kumi mwaka huu nchini kote, kulia ni Kamishna wa Kodi za Ndani Bw.Elaijah Mwandumbya. Kamishna wa TRA Bw. Alphayo Kidata akipata maelezo kutoka kwa Rehema Shayo Meneja wa Usajili TRA wakati akikagua utekelezaji wa uhakiki huo.

  ......................................................

  TRA kupitia kwa Kamishina Mkuu wa Ofisi hiyo wamezindua zoezi maalumu kwa ajili ya kuhakiki na kuboresha taarifa za usajili wa namba za utambulisho wa mlipa kodi (TIN) . Uzinduzi huo umefanywa na Kamishna Mkuu wa Ofisi hiyo Bw, Alphayo Kidata kwa kushirikiana na wafanyakazi wa ofisi hiyo mapema hii leo jijini Dar es salaam, hivyo kuanzia sasa zoezi hilo litakuwa endelevu katika mikoa yote nchini ya bara na visiwani .

  Kidata alisema kuwa lengo kubwa la uzinduzi wa zoezi hilo ni kubadili mfumo wa sasa wa kuhifadhi kumbukumbu za walipa kodi kwa kuweka mfumo mpya unaoendana na ukuaji wa teknolojia ambao utakuwa na walipa kodi wake wanaostahili kuwepo kwenye wigo.

  Aidha aliongeza kuwa mfumo huo utasaidia kuwaondoa walipa kodi hewa ,kuongeza ufanisi katika suala zima la usimamizi wa ukusanyaji kodi kwa kiwango cha juu na kuwezesha ulipaji kodi kuwa nafuu kwa mlipaji.

  Hata hivyo katika hatua nyingine Kidata ametoa wito kwa yeyote mwenye namba ya utambulisho wa mlipa kodi kufika katika ofisi za mamlaka hiyo ili kuweza kupata utaratibu wa zoezi zima jinsi linavyokwenda
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: KAMISHNA WA TRA AZINDUA KAMPENI YA KUHAKIKI NAMBA YA MLIPA KODI (TIN) Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top