728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, August 18, 2016

  JWTZ YANYAKUA VIKOMBE VITATU EAC KIGALI

  Mwanariadha siata kalinga akipokea kikombe cha mshindi wa tatu kwa riadha wanawake kutoka kwa mkuu wa Naibu Mkuu wa majeshi wa Uganda Luteni Generali Charles Angina (Picha na Selemani Semunyu)

  Mnadhimu mkuu wa Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania Luteni Generali Venance mabeyo akisalimiana na wachezaji wa timu ya Soka ya Tanzania wakati wa mchezo wa mwisho dhidi ya Rwanda Tanzania ilifungwa bao 1-0 na kushika nafasi ya tatu( picha na Selemani Semunyu)

  Viongozi waandamizi wa majeshi waliowakilisha wakati wa sherehe za kufungwa mashindano ya EAC kwa majeshi kiali nchini Rwanda kutoka kulia ni mkuu wa majeshi wa Rwanda Jenerali akifuatiwa na Mkuu wa majeshi wa Kenya Jenerali Samson Mwathethe(wa pili kulia),Mnadhimu mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Venance Mabeyo (Wapili kushoto) na Naibu mkuu wa majeshi wa Uganda Luteni Jenerali Charles Angina(picha na Selemani Semunyu)

   
  NA SELEMANI SEMUNYU JWTZ 

  JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA LIMEIBUKA NA VIKOMBE VITATU KATIKA MASHINDANO YA MAJESHI KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI YALIYOFANYIKIA KIGALI NCHINI RWANDA TANGU AGOSTI TANO HADI AGOSTI 17. 

  JWTZ ILIYOKUWA NA TIMU TANO ZA RIADHA,SOKA,KIKAPU,MPIRA WA MIKONO NA MPIRA WA PETE IMEFANIKIWA KUCHUKUA USHINDI WA KWANZA IKWA UPANDE WA MPIRA WA PETE HUKU IKISHIKA NAFASI YA TATU KWA MPIRA WA MIGUU NA RIADHA. 

  KWA UPANDE WAKE WAWAKILISHI WA TIMU HIZO ZA TANZANIA NASRA SULEIMAN AMBAYE PIA NI MCHEZAJI BORA WA MPIRA WA PETE NA DAMAS MAKWAYA WALOIKUWA NA HAYA YA KUSEMA MARA BAADA KUKABIDHIWA VIKOMBE HIVYO. 

  NAHODHA WA WA SOKA DAMAS MAKWAYA ALISEMA KATIKA MCHEZO WA MWISHO WALIZIDIWA MBINU LAKINI WANAIMANAI SAFARI IJAYO WATABORESHA ZAIDI KIKOSI NA KUWEZA KUFIKIA MALENGO YAO YA KUWA MABINGWA NA SIO MSHINDI WA TATU. 

  NASRA SULEIMAN ALISEMA TUZO NA KIKOMBE WALICHOPATA WALISTAHILI WATAJITAHIDI KATIKA MASHINDANO YAJAYO KUWEZA KUKILINDA NA KUFANYA VYEMA ZAIDI KWA NAFASI ZA USHINDI WA UFUNGAJI BORA NA HATA MLINZI BORA. 

  KWA UPANDE WA SOKA MSHINDI NI KENYA AKIFUATIWA NA RWANDA AMBAO WALIKUTANA KATIKA MCHEZZO WA MWISHO NA TANZANIA AMBAPO WALIIBUKA NA USHINDI WA BAO MOJA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: JWTZ YANYAKUA VIKOMBE VITATU EAC KIGALI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top