728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Friday, August 12, 2016

  JAMANI FOUNDATION KWA KUSHRIILIKIANA NA TEA YAENDELEA KUTOA MADAWATI KWA SHULE ZA MSINGI

  Mkurugenzi wa Jamani Foundation, Nirmala Pabari (kushoto) akikabidhi madawati Mameneja wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Tito Mganwa (kulia), Anne Mlimuka (wa pili kulia). Katikati ni Mwalimu Kasyupa kutoka Shule ya Msingi Yombo akiwakilisha kwa niaba ya waalimu wa shule zilizopokea msaada wa madawati 100.
  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Yombo wakiwa wamekaa katika madawati waliyokabidhiwa na taasisi ya Jamani Foundation. Kutoka kushoto, Mkurugenzi wa Jamani Foundation, Nirmala Pabari, Meneja wa TEA, Tito Mganwa na Anne Mlimuka.
  Meneja Ufadhili wa Miradi ya Elimu, Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Anne Mlimuk (kushoto), akikabidhi madawati yaliyotolewana JAMANI Foundation kupitia TEA kwa mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Umoja, Juto Komba.

  Meneja Ufadhili wa Miradi ya Elimu, Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Anne Mlimuk (kushoto), akikabidhi akizungumza katika hafla yakupokea madawati 100 kutoka taasisi ya Jamani Foundation.Mkurugenzi wa Jamani Foundation akizungumza katika hafla ya utoaji wa madawati 100 kwa Shule ya Msingi Yombo. 
  WanafunziwashuleyaMsingiyaMsingiUmojawakichezangomayaasili, kutumbuiza katika hafla ya makabithiano ya madawati.

  JAMII imetakiwa kujenga utaratibu wa kutunza vifaa vya misaada vinavyotolewa kwa ajili ya shule ili viweze kudumu na kusaidia wanafunzi kwa muda mrefu.

  Ushauri Huo ulitolewa jana na Meneja wa Uhamasishaji na Wateja wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Tito Mganwa wakati wakikabidhiwa madawati 100 yaliyotolewa na Jamani Foundation kwa shule za msingi Umoja na Yombo za jijini Dar es Salaam.

  Alisisitiza umuhimu wa shule na wazazi kuwajengea watoto utaratibu wa kuthamini na kutunza vifaa wanavyopewa ili viweze kuduma na kunufaisha wanafinzi wengi zaidi kwa muda mrefu.

  “Madawati haya 100 yamegharimu 12m/-, hii inaonyesha ni jinsi gani wenzetu wa Jamani Foundation wanathamini mahitaji yetu nasi basi kuonyesha shukrani yetu tunapaswa kuyatunza ili yadumu na wenzetu wengine wafaidike pia na msaada huu” alisema Mganwa.

  Aliishukuru Jamani Foundation kwa ushirikiano wao na Mamlaka ya Elimu katika kuhakikisha kuwa wanaondoa kero zinazoikabili sekta ya elimu nchini ili kuhakikisha ubora wa elimu unazingatiwa.

  Amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikishirikiano nayo katika kukabiliana na kero ya upungufu wa madawati na kwa sasa wanategemea kuanza ushirikiano katika mradi wa ujenzi wa vyoo ili kutunza afya za wanafunzi mashuleni.

  Akizungumza wakati wa kuwakabidhi TEA madawati hayo, Meneja wa huduma za jamii wa Jamani Foundation, Bi Nirmala Pabari alisisitiza umuhimu wa mashirika na asasi mbalimbali kusaidia jamii ili kuboresha maisha.

  Alisema wataendelea kushirikiana na serikali katika maeneo mbali mbali kulingana na mahitaji na uwezi wao lengo lao likiwa ni kuhakikisha kuwa jamii inaishi katika mazingira bora ya upatikanaji wa huduma muhimu za jamii.

  Akipekea madawati hayo, Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Umoja, Bw Dyuto Komba alisema watatumia utaratibu wa kugawa kila dawati kwa mwanafunzi na kuandikishana na wazazi wao ili kujenga dhana ya uwajibikaji.

  “Kama tulivyofanya kwenye kugawa kitabu, na kwa madawati hivyo hivyo, yatapewa namba na majina ambapo kila mwanafunzi atapaswa kulitunza na likiharibika mzazi au mlezi atawajibika kwa matengenezo” alisema.


  Alisema baada ya msaada huo, shule yake haina tena shida ya madawati na kusema changamoto waliyonayo ni uhaba wa madarasa hasa kutokana na kuongezeka kwa usajili wa wanafunzi wa shule ya awali na msingi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: JAMANI FOUNDATION KWA KUSHRIILIKIANA NA TEA YAENDELEA KUTOA MADAWATI KWA SHULE ZA MSINGI Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top