728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, August 16, 2016

  Ilala Boys mabingwa Airtel Rising Stars Ilala


  Timu ya Simba Queen wakishangilia baada ya kushinda mechi ya fainali ya wasichana katika Wilaya ya Ilala juzi katika michuano ya U-17 Airtel Rising Stars iliyokuwa ikichezwa katika uwanja wa Karume.
  Mshambulaiji wa Timu ya Bombom SC, Jamal Abdul (Katikati) akipambana na mabeki wa Timu ya Ilala Boys wakati wa mechi ya Fainali ya U-17 ARS kwa wavulana katika uwanja wa Karume juzi. Timu ya IlalaBoys ilishinda 3-0


  Mbunge wa Ilala (CCM) Mussa Zungu akimkabidhi kombe Nahoza wa Timu ya Ilala Boys, Rajabu Ally baada ya kushinda mechi ya fainali kwa wavulana Wilaya ya Ilala juzi katika michuano ya U-17 Airtel Rising Stars iliyokuwa ikichezwa katika uwanja wa Karume.Ilala Boys ilishinda 3-0 dhidi ya Bombom.


  Mbunge wa Ilala (CCM) Mussa Zungu akimkabidhi kombe Nahoza wa Timu ya Simba Queen, Hadija Ally baada ya kushinda mechi ya fainali ya wasichana Wilaya ya Ilala juzi katika michuano ya U-17 Airtel Rising Stars iliyokuwa ikichezwa katika uwanja wa Karume.Simba Queen ilishinda 5-0 dhidi ya Ilala.
  Timu ya wavulana ya soka Ilala Boys ya kimkoa wa Ilala jana imetwaa uchampioni wa michuano ya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Aitel Rising Stars kwa kuwafunga Bom Bom FC 3-0 kwenye uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam.

  Kwa upande wa wasichana timu ya Simba Queens ndio iliyotawazwa mabingwa kwa kushinda timu ya Ilala Queens kwa magoli 5-0 katika mchezo mkali uliovuta hisia za watamazaji waliojitokeza kushuhuduia mtanange huo.

  Katika mchezo wa wavulana, timu ya Ilala Boys walionyesha dalili za ushindi mapema baada ya kuanza mchezo kwa mashambulizi mfululizo na walichukua dakika sita kuandika bao ya kwanza likifungwa na Rajabu Ally baada ya kungona vyema na mshambuliaji mwenzake Issa Abushiri.

  Dakika ya saba ya mchezo Ilala Boys waliandika bao la pili baada kupingwa mpira wa kona na mabeki wa Bom Bom FC kushindwa kuokoa. Bao la tatu lilipatikana dakika ya 42 ya kipindi cha pili baada ya kupingwa mpira mrefu huku mabeki wa Bom Boma wakisimama wakifikiri mfungaji, Issa Abushiri ameotea.

  Akikabidhi vikombe kwa washindi, Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu amewataka wachezaji waliochaguliwa kuiwakilisha Mkoa wa Ilala vyema kwenye fainali za Taifa za Airtel Rising Stars zinatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba mwaka huu. ‘Mkoa wa Ilala ulikuwa kila mwaka ukifanya vizuri kwenye mashindano, nina imani nanyi mtaendelea kulinda heshima ya mkoa wetu, alisema Zungu. Zungu pia alitoa pongezi kwa Kampuni ya Airtel kwa kutoa fursa kwa vijana kuonyesha vipaji vyao vya kandanda.

  Naye Meneja Huduma za jamii wa Airtel Tanzania Hawa Bayumi alizipongeza timu zote kwa kushiriki na kuwaasa wachezaji kulinda na kuviendeleza vipaji vyao ambavyo ni hazina kwa taifa. Aliseema lengo lilikuwa ni kuibua vipaji na kuwaasa vijana ambao hawakuchaguliwa kutokata tama na badala yake wajinge kufanya vizuri mwakani.

  Kukamilika kwa michuano hiyo mkoa wa Ilala ndio kunafunga pazia la Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa huo iliyoanza kutimua vumbi mwezi uliopita.

  Mashindano ya Airtel Rising Stars ambayo mwaka huu yanashirikisha mikoa ya Ilala, Kinondoni, Temeke, Morogoro, Mbeya, Mwanza, Zanzibar, Lindi na Arusha na zinatarajiwa kuingia kwenye hatua nyeti ya fainali za Taifa iliyopangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, kuanzia Septamba 6 hadi 11 nmwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Ilala Boys mabingwa Airtel Rising Stars Ilala Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top