728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, August 9, 2016

  HUYU HAPA NDIYE MKURUGENZI MPYA WA IDARA YA HABARI (MAELEZO).

   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimtangaza Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) ambaye pia ni Msemaji wa Serikali Bw. Hassan Abbas (kushoto) anayechukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Assah Mwambene aliyehamishiwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa.PICHA NA MICHUZI JR-MMG.
   Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) ambaye pia ni Msemaji wa Serikali Bw. Hassan Abbas akieleza mikakati yake ikiwemo kuongeza mbinu za Mawasiliano kati ya serikali na wananchi ili kuchochea maendeleo katika kipindi cha serikali ya awamu ya tano. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye.
  Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye alipokuwa akimtangaza Mkurugenzi mya wa Idara ya Habari (MAELEZO) ambaye pia ni Msemaji wa Serikali Bw. Hassan Abbas (kushoto) anayechukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Assah Mwambene aliyehamishiwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: HUYU HAPA NDIYE MKURUGENZI MPYA WA IDARA YA HABARI (MAELEZO). Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top