728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, August 11, 2016

  HOSPITALI ZA DAR ES SALAAM KUNUFAIKA NA PROGRAMU YA 5'S KAIZEN

  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH), Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ilala ya Amana pamoja na Hospitali ya Mwananyamala kupitia programu ya 5’S-KAIZEN zimefanikiwa kuboresha huduma ya afya kwa wagonjwa wanaofika kupata matibabu katika hopspitali hizo.

  Programu ya 5’ S- KAIZEN inafadhiliwa na Serikali ya Japan chini ya Shirika la ushirikiano wa kimataifa JICA inalenga kumuandalia mfanyakazi wa afya hatua nzuri ya kutumia kiwango cha juu cha ujuzi na maarifa ikiwemo Sasambua, Seti, Safisha, Sanifisha pamoja na Shikilia (5’ S-KAIZEN).

  Akizungumza kuhusu program hiyo msimamizi kutoka Ofisi ya Mradi wa Maendeleo ya Rasilimali watu wa JICA, Hisahiro Ishijima alisema kuwa lengo la programu hiyo ni kukuza na na kuanzisha maarifa ya njia ya uboreshwaji wa huduma za afya katika nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Tanzania.

  Amesema kuwa usimamiaji wa mifumo ya utoaji huduma hospitalini unakabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana na ukosefu wa rasilimali tiba, na kuongeza kuwa changamoto hiyo inayopaswa kutatuliwa ili kuboresha huduma bora za matibabu.

  “kanuni ya S Tano(5’S) ni nyenzo ya usimamiaji inayotumika kama njia ya msingi na inayotekelezeka hatua kwa hatua ili kuimarisha ubora na usalama katika aina zote za mpangilio ya kazi ikiwemo sekta ya afya”Alisema

  Kwa upande wake Afisa Muuguzi Mwandamizi katika hospitali ya Amana, Evelyne Rwezaura alisema kuwa Hospitali hiyo inatekeleza programu ya 5’ S-KAIZEN ambapo kwa sasa hospitali hiyo imefanikiwa kuwa na mazingira mazuri ikiwemo upangaji mzuri wa mafaili ya wagonjwa na dawa.

  “Tangu kuanza kwa mkakati huu wa mpango wa 5’S mazingira ya hospitali yamebadilika ukilinganisha na mazingira ya awali kwani kwa sasa kumekuwa na mpangilio mzuri kuanzia mafaili ya wagonjwa, dawa na usafi kwa ujumla ikiwemo utupaji wa taka hatarishi” aliongeza Rwezaula.

  Naye Idrisa Mintanga, ambaye ni mgonjwa aliyelazwa katika hospitali hiyo alisema kwa sasa hospitali hiyo ya Amana kumekuwa na mabadiliko makubwa ukilinganisha na awali kuanzia mapokezi, usafi wa mazingira kwa ujumla, muda wa kusubiria umeimarishwa na kuuomba uongozi wa hospitali hiyo kuzidi kuimarisha huduma zake kwani kunamfanya mgonjwa kuona kuwa anadhaminiwa.

  Aidha, Afisa Muuguzi katika wodi ya Kibasila katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alisema mbali na pamoja na changamoto zilizopo za vitendea kazi, upungufu wa mafunzo kwa wafanyakazi, mpango wa KAIZEN umeweza kutatua changamoto za usimamiaji ubora kwa ujumla katika hospitali hiyo.
   
  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
  DAR ES SALAAM
  10/08/2016
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: HOSPITALI ZA DAR ES SALAAM KUNUFAIKA NA PROGRAMU YA 5'S KAIZEN Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top