728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, August 23, 2016

  HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI YAPOKEA MSAADA WA MAGARI MAWILI YA KUBEBEA WAGONJWA YENYE THAMANI YA SH MIL 80 KUTOKA UBALOZI WA JAPAN  Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa kwanza kushoto akionyesha funguo ya gari la kubebea wagonjwa baada ya kupokea msaada wa magari mawili kutoka Serikali ya Japan leo jijini Dar es salaam kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa ya taifa Muhimbili, kulia ni Balozi wa Japan Bw. Masaharu Yoshida nae akionyesha funguo mojawapo ya gari hizo.

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akikata utepe kuashiria kupokea gari la kubebea watoto katika Hospitali ya Rufaa ya taifa Muhimbili kutoka kampuni ya Bango Sangho na kulia ni Mwenyekiti wa kampuni hiyo Bw. Niladri Chowdhury.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu aliyepiga katikati akifurahia jambo na watoto walio katika Hospitali ya Rufaa ya taifa Muhimbili wakati alipopokea gari la kubebea watoto katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam na kulia ni Mwenyekiti wa kampuni ya Bango sangho Bw. Niladri Chowdhury.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu aliyesimama akiongea na wajumbe ya bodi ya udhamini ya Hospitali ya Rufaa ya taifa Muhimbili wakati alipozindua bodi hiyo leo jijini Dar es salaam na wa kwanza aliyekaa kushoto ni Mwenyekiti wa bodi hiyo Dkt. Charles Majinge

  Habari/Picha Na Ally Daud

  Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Muhimbili (MNH) imepokea msaada wa magari mawili ya kubebea wagonjwa yenye thamani ya shilingi milioni 80 kutoka ubalozi Wa Japan kwa ajili ya kusaidia utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

  Akipokea msaada wa magari hayo leo jijini Dar es salaam Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa anashukuru kwa msaada huo kwani utarahisisha huduma kwa wagonjwa wa hospitali hiyo.

  "Nashukuru kwa msaada uliotolewa na serikali ya Japan na wasichoke kutusaidia katika kuboresha sekta ya Afya nchini" alisema Mhe. Ummy.

  Kwa upande wa Balozi Wa Japan Bw. Masaharu Yoshida amesema kuwa hawatachoka kutoa msaada kwa Tanzania ili kuboresha sekta ya afya na kuweka mahusiano bora kati ya Japan na Tanzania. " Hatutachoka kutoa msaada kwa Tanzania kwani tunaboresha sekta ya afya na kudumisha mahusiano yetu" alisema Bw. Yoshida

  Kwa wakati huohuo Waziri Ummy amepokea gari lingine la kuwabebea watoto kutoka kwa kampuni ya Bango Sangho ili kurahisisha kuwapeleka katika kliniki mbalimbali jijini Dar es salaam.

  Akikabidhi gari hilo Mwenyekiti wa kampuni ya Bango Sangho Bw. Niladri Chowdhury amesema kuwa wameamua kutoa msaada huo ili kuwarahisishia watoto kupelekwa kliniki kwa haraka pindi inapohitajika na kuokoa maisha yao.

  Mbali na hayo Waziri Ummy pia amezindua bodi ya udhamini katika hospitali ya Muhimbili amabayo itadumu kwa muda wa miaka mitatu ili kufanya huduma za ya hospitali hiyo kuwa bora zaidi kwa maendeleo ya sekta ya afya nchini.

  Akizungumza katika uzinduzi Wa bodi hiyo Mhe. Ummy amesema kuwa bodi hiyo iwe ya kiutendaji na kutatua matatizo ya wagonjwa na sio kua kero kwa wafanyakazi na wananchi.

  Aidha Waziri Ummy ameitaka bodi hiyo kufanya kazi kwa kushirikiana na wizara pamoja na menejimenti ya hospitali hiyo ili kuleta huduma bora za kiafya kwa maendeleo ya taifa letu kwa ujumla.

  Kwa upande wa Mwenyekiti mpya wa bodi ya udhamini ya MNH Dkt. Charles Majinge amesema kuwa amepokea nafasi hiyo kwa mikono miwili na kuahidi kuleta mabadiliko katika sekta ya afya nchini kwa kushirikiana na Wizara.

  “Licha ya changamoto zilizopo nimeipokea nafasi hii kwa mikono miwili na kuhaidi kuleta mabadiliko katika sekta ya afya nchini kwa mda uliopangiwa ili kuleta maendeleo ya huduma bora kwa jamii.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  1 comments:

  1. Fanya marekebisho:Mwenyekiti wetu ni Profesa Charles Majinge

   ReplyDelete

  Item Reviewed: HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI YAPOKEA MSAADA WA MAGARI MAWILI YA KUBEBEA WAGONJWA YENYE THAMANI YA SH MIL 80 KUTOKA UBALOZI WA JAPAN Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top