728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Sunday, August 7, 2016

  Friedkin Conservation Fund na African Wildlife Trust wadhamini Rock City Marathon


  IKIWA ni sehemu ya mkakati wa kupambana na ujangili pamoja na kutangaza utalii wa ndani kampuni za Uhifadhi za Friedkin Conservation Fund (FCF) na African Wildlife Trust (AWT) zimeamua kudhamini Rock City Marathon inayotarajiwa kufanyika Septemba 25 kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam jana kuhusiana na udhamini huo wa miaka mitatu, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hizo Bw Pratik Patel alisema kampuni mzake zitatumia mbio hizo kuzindua kampeni yao inayofahamika “*Okoa Wanyama Wetu*; *Kataa Ujangili”*

  “Tutatumia Rock City Marathon kutangaza kampeni yetu ya kupinga ujangili
  itakayofanyika katika baadhi ya majiji ulimwenguni.,’’ alibainisha Pratik. Alisema kampeni hiyo ya “*Okoa Wanyama Wetu*; *Kataa Ujangili”* itaanza nanmatembezi yatakayofanyika Septemba 24 mwaka huu jijini Arusha, Moshi na Dar es Salaam yakifuatiwa na mbio hizo Septemba 25, Uwanja wa CCM Kirumba.

  “Tuliamua kudhamini Rock City Maratahon kwa kuwa lengo la mbio hizi ni
  kutangaza utalii wa ndani na sisi tuliona kwamba huo utalii unaotangazwa
  ili uwe na tija zaidi unategemea uwepo wa maliasili. Na ni wazi kwamba
  uwepo wa maliasili hizi unategemea sana jitihada za kweli katika uhifadhi
  wake! Na hapo ndipo hasa utatukuta sisi ,’’ alisema.

  Wakizungumza kwenye uzinduzi wa mbio hizo jijini Mwanza hivi karibuni, Mkuu wa mkoa huo John Mongella na Mkuu wa mkoa wa Simiyu ambae pia ni Rais wa chama cha riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka walipongeza wadhamini wa mbio hizo zikiwemo kampuni za Friedkin Conservation Fund (FCF) na African Wildlife Trust (AWT) kwa kuunga mkono jitahada za serikali  katika kutangaza utalii wa ndani pamoja na kupambana na ujangili hapa nchini.

  Pamoja na pongezi hizo pia viongozi hao wa walikuwa wa kwanza kujisajili
  kushiriki Rock City Marathon huku wakiahidi kuhakikisha kwamba mbio
  zinapata washiriki wa kutosha sambamba na wadhamini kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa.

  Mbali na kampuni za Freidkin Conservation Fund na African Wildlife
  Trust,wadhamini wengine wa mbio hizo ni pamoja na  Mwanza Hotel, Nyanza Bottlers Limited, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Real PR
  Solutions na kampuni ya Fabec.

  Akizungumzia mbio hizo Mratibu kutoka kampuni ya Capital Plus Bw Mathew Kasonta alisema Rock City Marathon zitahusisha makundi matano yaani mbio za kilomita 21 kwa wanaume na wanawake, kilomita 5 kwa ngazi ya ‘corporate’, kilomita 3 kwa ajili ya walemavu na zile za wazee umri zaidi miaka 55 na kuendelea pamoja na kilomita 2 kwa ajili ya watoto umri kati ya miaka 7 hadi 19.

  Pia litoa wito kwa wakazi wa jiji la Mwanza na mikoa jirani kujisajili kwa
  kuchukua fomu katika vituo kadhaa vikiwemo Ofisi za michezo wilaya zote za
  mkoa wa Mwanza, Ofisi zote za riadha mikoa ya Geita, Simiyu na
  Shinyanga,   Uwanja wa Nyamagana,  Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino  Mwanza, Kituo cha michezo Malya na Shule ya Kimataifa ya Isamilo,

  “Kwa upande wa Dar es Salaam Fomu za ushiriki pia zinapatikana katika ofisi za Kampuni ya Capital Plus International zilizopo ghorofa ya tatu jengo la ATC, jijini Dar es, Salaam na vituo vingine vitaendelea kutangazwa hivi
  karibuni,” alihitimisha.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Friedkin Conservation Fund na African Wildlife Trust wadhamini Rock City Marathon Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top