728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, August 16, 2016

  Dr.Amon Mkoga Foundation wakabidhi madawati 90 kwa wilaya ya Tabora mjini.


  Mwenyekiti wa Taasisi ya Dr.Amon Mkoga Foundation Ndugu.Amon Mkoga akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Isike kulia ni Amina Rajabu na kushoto ni na James Shija.
  Afisa Tawala Wilaya ya Tabora mjini Mhe. Sweetbert Nkuba, (kushoto) akipokea moja ya madawati 90 yaliyotolewa na Dr.Amon Mkoga Foundation na kukabidhiwa kwake na mwenyekiti wa Taasisi hiyo Ndugu.Amon Mkoga(kulia). Anayeshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde Msika ambao ni wadhamini wa kampeni hiyo iitwayo “Simama Kaa” Mwenyekiti wa Taasisi ya Dr.Amon Mkoga Foundation Ndugu.Amon Mkoga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Isike Manispaa ya Tabora.

  Taasisi ya Dr.Amon Mkoga Foundation imetoa msaada wa madawati 90 yenye thamani ya shilingi milioni 5.5 kwa shule za msingi katika manispaa ya Tabora, ikiwa ni mchango wa Taasisi hiyo katika kuisaidia serikali kukabiliana na upungufu wa madawati katika shule za msingi nchini.

  Akizungumza leo katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi ya mkuu wa wilaya Tabora mjini , Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Ndugu Amon Mkoga amesema mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya taasisi hiyo ya kuunga mkono jitihada mbalimbali za kuleta maendeleo nchini.

  “Mchango huu ni sehemu ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na Dr.Amon Mkoga Foundation katika kusaidia utekelezaji wa miradi yenye tija kubwa kwa jamii. Tunaamini kwamba kupitia msaada huu, Taasisi yetu inatoa mchango wake katika kujenga viongozi wa baadaye wa taifa hili na wanataluuma mbalimbali wakiwamo madaktari, wahandisi na wengineo, “amesema Mkoga.

  Makabidhiano yalihudhuriwa na Afisa Tawala Wilaya ya Tabora mjini Mhe. Sweetbert Nkuba ambaye alisema madawati hayo 90 yataboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto katika Mkoa wa Tabora na kutoa wito kwa wadau wengine kuunga mkono zoezi hilo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Dr.Amon Mkoga Foundation wakabidhi madawati 90 kwa wilaya ya Tabora mjini. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top