728x90 AdSpace






 • Habari za hivi Punde

  Thursday, August 18, 2016

  DC KISHAPU AFANYA KIKAO NA WAFUGAJI WA WILAYA

  Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Taraba akizungumza na makundi ya wafugaji wa wilayani humo (hawapo pichani) katika kikao cha kujadili maendeleo ya sekta hiyo na kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili. 

   Tukio hilo limefanyika leo katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ambapo mkuu huyo wa wilaya aliwataka kushiriki katika shughuli za maendeleo ya wilaya. 

   Taraba alisema kuwa wafugaji wana mchango mkubwa katika maendeleo ya wilaya, mkoa na taifa kwa ujumla hivyo wamuunge mkono ili kuwaletea wananchi maendeleo. 

   Aliwaomba kuchangia shughuli za maendeleo hususan katika utengenezaji wa madawati ili yasambazwe katika shule zilizopo wilayani humo ili watoto wasikae chini. Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa Kishapu ina mnada ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini kote hivyo wafugaji wautumie kuleta maendeleo ya wilaya na taifa. 

   Hata hivyo, aliwakumbusha kutumia wataalamu katika kuboresha ufugaji wao uwe wa kisasa zaidi yaani kufuga na siyo kuishi na mifugo kama inavyokuwa siku zote.
  Wafugaji wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Nyabaganga Taraba alipokuwa akizungumza nao katika kikao cha kujadili maendeleo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: DC KISHAPU AFANYA KIKAO NA WAFUGAJI WA WILAYA Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top