JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


Balozi wa Palestina Achangia Damu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo.

Share This
 Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Hazem Shabati akichangia damu leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kulia ni mtaalamu kwa kutoa damu katika hospitali hiyo, Sabastian Magulu. 
 Mkuu wa Idara ya Maabara Mkuu katika hospitali  hiyo, Alex Magesa akijadiliana jambo na Balozi huyo baada ya kumaliza kuchangia damu leo.

Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Hazem Shabati akijisajili kabla ya kuchangia damu leo katika hospitali hiyo. Kushoto ni Msajili wa damu, Titus Mhokole. Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Hazem Shabati amewataka Watanzania kuwa na tabia ya kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu.

Balozi Shabati amefika leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili kuchangia damu na kuwahamasisha watu wajitokeze kwa wingi ili kuchangia damu.

Amesema kila mtu ana wajibu wa kuchangia damu kwa kuwa ni muhimu kwa maisha ya wagonjwa wenye matatizo mbalimbali ya kiafya.

Pia, Balozi Shabati amesema lengo la kuchangia damu ni kudumisha uhusiano kati ya Tanzania na nchi yake ambao ni wa muda mrefu na wa kihistoria.

 Katika hatua nyingine, Ofisa Uhusiano wa hospitali hiyo, Neema Mwangomo amesema kwa wastani hospitali hiyo inakusanya chupa 40 hadi 50 kwa siku, lakini mahitaji kwa siku ni chupa 80 hadi 100.

Amesema makundi makubwa yanayohitaji damu kina mama wajawazito, watoto wenye saratani, majeruhi wa ajali na wagonjwa wanaotakiwa kufanyiwa upasuaji.

Mwangomo amesema mwanaume mwenye umri wa miaka 18 hadi 65 ndiye anapaswa kuchangia damu wakati mwanamke ni miaka 18 hadi 62.

Amesema kigezo cha pili ni mtu anayechangia damu anapaswa kuwa na uzito wa kilo 50 na kuendelea na kwamba mtu anapaswa kuwa na wingi wa damu kuanzia asilimia 85.

Mwanamke anaweza kuchangia damu mara tatu kila baada ya miezi minne wakati mwaume mara nne kila baada ya miezi mitatu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad