728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Saturday, July 30, 2016

  WAZIRI NAPE NNAUYE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA YA JOSEPH EMILIO SENGA.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Joseph Emilio Senga na wanahabari wote nchini kufuatia kifo cha aliyekuwa mpiga picha mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima na mwanahabari mkongwe Joseph Emilio Senga kilichotokea tarehe 27 Julai, 2016 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.

  Katika salamu zake Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) amesema tasnia ya habari imempoteza mtu aliyetoa mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya tasnia ya habari nchini.

  “Joseph Senga alikuwa mwanahabari shupavu na hodari, ambaye siku zote alisimama kidete kupigania maendeleo ya tasnia ya habari na kutenda haki katika tasnia hiyo.

  “Napenda kutoa salamu zangu za pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote wa marehemu” 

  Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) pia amewaombea wote walioguswa na kifo cha Joseph Emilio Senga kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki cha kuondokewa na mpendwa wao.

  RAHA YA MILELE UMPE EHE BWANA, NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE 

  APUMZIKE KWA AMANI

  AMINA.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WAZIRI NAPE NNAUYE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA YA JOSEPH EMILIO SENGA. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top