728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Monday, July 18, 2016

  Waziri Mkuu Mgeni Rasmi Kongamano la ushiriki wa watanzania katika uwekezaji.

   Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Dk.Hamis Mwinyimvua (kulia) akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kongamano la siku mbili la ushiriki wa watanzania katika uwekezaji ili kuiwezesha serikali kuweka mipango madhubuti ya kuhakikisha waanchi wake wanashiriki kikamilifu katika uchumi wa nchi yao.Kulia kwake ni Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Bengi Issa.
  Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Bengi Issa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari na kuwahimiza watanzania kushiriki kikamilifu katika kongamano la siku mbili la ushiriki wa watanzania katika uwekezaji ili kuiwezesha serikali kuweka mipango madhubuti ya kuhakikisha waanchi wake wanashiriki kikamilifu katika uchumi wa nchi yao.Picha na Daudi Manongi,MAELEZO.


  Na Daudi Manongi-MAELEZO

  SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imeandaa kongamano kongamano la siku mbili la uwekezaji litakalojadili mipango madhubuti ya kuhakikisha Watanzania wanashiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa nchi yao.

  Kongamano hilo linatarajia kufanyika katika ukumbi wa Benki Kuu Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 21 -22 Julai mwaka huu. Hayo yamesemwa leo Jijiji Dar es Salaam na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt.Hamis Issa wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu kongamano hilo.

  Dkt. Issa alisema Serikali imepitisha Sera ya ushiriki wa watanzania katika sekta ya Mafuta na Gesi asilia, hatua ambayo itasadia wananchi wazawa kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa nchi yao.

  “Msukumo mkubwa wa serikali kwa sasa ni kuongeza ushiriki katika uwekezaji unaochochewa na ugunduzi mkubwa wa gesi asilia katika kina kirefu cha bahari ambao utaweza kuwanufasha Watanzania” alisema Dkt. Issa.

  Aidha alisema kuwa kutokana ushiriki huo wa Watanzania kuwa suala mtambuka na agenda endelevu, Serikali iliiagiza Baraza la Taifa la Uwezeshaji kuanzisha Idara ya ushiriki wa watanzania katika uwekezaji ambayo imeanza kutekeleza majukumu yake mwezi Novemba mwaka 2015.

  Kwa upande wake Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji, Beng’i Issa alisema kuwa katika kongamano hilo linatarajia kushirikisha jumla ya wajumbe 350 wakiwemo wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi, Watendaji wa Serikali Kuu na halmashauri za Miji na Majiji.

  Akizungumzia kuhusu manufaa ya kongamano hilo, Beng’i alisema Watanzania watanufaika zaidi kwa kuwa wataongeza ujuzi na uzoefu katika kushirikiana na wafanyabiashara wakubwa waliopo nje ya nchi wanaojihusisha na sekta za mafuta, gesi, kilimo, fedha, bima, ujenzi na manunuzi ya umma.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Waziri Mkuu Mgeni Rasmi Kongamano la ushiriki wa watanzania katika uwekezaji. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top