728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, July 28, 2016

  Waziri Mkuu Majaliwa apokea madawati kutoka kwa Balozi wa Kuwait na Jumuiya ya Mabohora


  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na Balozi wa Kuwait Mhe Jaseem Al Najem wakiwa wamekaa katika madawati ambayo yametolewa na Ubalozi wa Kuwait wakati wa hafla ya makabidhiano ya madawati 300 ikiwa ni sehemu ya madawati 600 ambayo ubalozi huo umeahidi kutoa kwa Serikali mapema hii leo katika shule ya Msingi Chamanzi iliyopo wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabohora nchini Bw. Zainudin Adamje wakati wa hafla ya makabidhiano ya madawati 105 kati ya 250 ambayo Jumuiya hiyo imeahidi kutoa kwa serikali mapema hii leo katika shule ya Msingi Chamanzi iliyopo wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akimkabidhi hundi Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa hafla ya makabidhiano madawati ikiwa ni fedha zilizochangwa na watumishi wa wizara hiyo ikiwa sehemu ya kutekeleza agizo la Rais Mhe. John Magufuli mapema hii leo katika shule ya Msingi Chamanzi iliyopo wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam .
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimkabidhi hundi Msimamizi wa kikosi Kazi cha Utengenezaji Madawati Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza John Masunga wakati wa hafla ya makabidhiano madawati mapema hii leo katika shule ya Msingi Chamanzi iliyopo wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam .
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akifurahia jambo wakati wa hafla ya makabidhiano madawati ilyofanyika mapema hii leo katika shule ya Msingi Chamanzi iliyopo wilaya ya Temeke jijini dare s Salaam, kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabohora nchini Bw. Zainudin Adamje na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga.

  Picha zote na Eliphace Marwa -Maelezo
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Waziri Mkuu Majaliwa apokea madawati kutoka kwa Balozi wa Kuwait na Jumuiya ya Mabohora Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top