728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, July 28, 2016

  WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA MAJALIWA ATAKA MABARAZA YA MADIWANI KUFANYA MAPITIO YA UPUNGUFU VYA VYUMBA VYA MADARAKA KATIKA HALMASHAURI NCHINI.


  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

  WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa ametoa maagizo kwa Mabaraza ya Madiwani nchini kufanya mapitio katika shule zote za Halmashauri ili kujua upungufu wa madarasa na kuanza mkakati wa utekelezaji wa ujenzi wake.

  Aliyasema hayo leo wakati akipokea mchango wa madawati kwa shule ya msingi Chamazi kutoka Wizara Ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais la upatikanaji wa madawati katika shule za msingi na sekondari nchini.

  Mhe. Majaliwa alisema suala la upatikanaji wa madawati linakwenda sambamba na ujenzi wa madarasa hivyo ni wajibu wa kila halmashauri kuweka mkakati wa ujenzi wa vyumba vya madarasa kwani elimu bora ni pamoja na kuwa na mazingira rafiki ya kusomea.

  ‘Mbali na utekelezaji wa agizo la Rais juu ya mkakati wa upatikanaji wa madawati, suala hili linakwenda sambamba na ujenzi wa madarasa hivyo Serikali imeanza utekelezaji wa ujenzi huo kwa maeneo machache hivyo ni jukumu la halmashauri kuhakikisha mnaandaa mikakati ya kuongeza vyumba vya madarasa’ alisema Majaliwa.

  Aidha Waziri Mkuu Majaliwa alisema kuwa Serikali imeanza mkakati wa utekelezaji wa mpango wa kutumia mfumo mpya wa upandishaji madaraja walimu kwa kuwa mfumo wa uliuotumika awali haukuwa na tija kwa maslahi ya walimu nchini.

  Akipokea madawati hayo Waziri mkuu alisema kuwa anajua shida iliyopo ya upungufu wa madawati katika wilaya ya Temeke hivyo na kugawa madawati hayo katika shule tatu zilizopo katika Wilaya hiyo ikiwemo shule ya msingi Chamazi, shule ya msingi Mbande pamoja na shule ya msingi Majimatitu .

  Kwa upande wake Waziri wa Wizara Ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga alisema wizara yake ina jukumu la kuhakikisha inaitangaza nchi ili kuvutia wawekezaji na kukuza uchumi wa nchi, na kuongeza kuwa elimu bora ni msingi imara katika kufanikisha hilo.

  Waziri Mahiga alisema Ubalozi wa Kuwait nchini pamoja na Jumuiya ya Mabohora wameikabidhi Serikali jumla 405 ili kuunga mkono jitihada za Rais ikiwemo .“Serikali ya Kuwait kupitia Ubalozi wake hapa nchini wametoa madawati 300 na kuahidi kutoa mengine 300 na Jumuiya ya Mabohora nao wamechangia madawati 105” alisema Balozi Mahiga.

  Kwa mujibu wa Waziri Mahiga alisema watumishi wa Wizara yake walichanga kiasi cha Tsh. Milioni 100 ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha umma ili kuhamasisha umma kuhusu zoezi la upatikanaji wa madawati katika shule za msingi na Sekondari nchini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA MAJALIWA ATAKA MABARAZA YA MADIWANI KUFANYA MAPITIO YA UPUNGUFU VYA VYUMBA VYA MADARAKA KATIKA HALMASHAURI NCHINI. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top