728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Thursday, July 21, 2016

  Waziri Mahiga azungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mkutano wa AU

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mapema jana mchana kuhusu Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika uliomalizika hivi karibuni nchini Rwanda. Katika mkutano huo Mhe. Waziri alielezea mambo mbalimbali yaliyojadiliwa katika Mkutano huo ikiwemo suala zima la Haki za Wanawake katika kufanya maamuzi, kupata nafasi za Uongozi na kushirikishwa kwenye utatuzi wa migogoro mbalimbali Barani Afrika. Kaulimbiu ya mkutano huo ilihusu "Haki za binadamu hususan za Wanawake". Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Wizarani, Bi. Mindi Kasiga. 
  Dkt. Mahiga akionyesha kwa waandishi wa habari Hati yake ya Kusafiria (passport) aliyopatiwa wakati wa mkutano wa AU. Hati hiyo imeanzishwa na Umoja wa Afrika kwa lengo la kuimarisha umoja na kurahisisha mawasiliano. Kulia ni Bi. Kasiga. 
  Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri Mahiga kwenye mkutano uliowakutanisha naye. Picha na Reginald Philip
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Waziri Mahiga azungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mkutano wa AU Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top