728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Sunday, July 17, 2016

  WAFANYAKAZI MKOA WA MANYARA WATAKIWA KUPIMA AFYA ZAO MARA KWA MARA.

  Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Eliamkim Maswi (kushoto) akipimwa afya yake mjini Babati na mtumishi wa hospitali ya mkoa huo John Martin, kwenye kikao cha kuimarisha afua za ukimwi mahali pakazi.
   
  Wafanyakazi wa Mkoa wa Manyara, wametakiwa kupima afya zao mara kwa mara ili kujitambua namna walivyo katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku ya kuhudumia jamii ya eneo lao.

  Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Eliakim Maswi aliyasema hayo jana mjini Babati wakati akizungumza kwenye kikao cha kuimarisha afya za ukimwi mahali pakazi iliyotolewa kwa watumishi wa ofisi ya mkuu wa mkoa huo. Maswi alisema kuwa lengo lao ni kuhakikisha mtumishi wa mkoa huo asiingie kwenye hatari ya kuambukizwa virusi vya ukimwi (VVU) na kama amekwisha ambukizwa asinyanyapaliwe na kusiwe na kifo kitokanacho na ukimwi.

  Alisema japokuwa hali ya maambukizi ya VVU kwa mkoa wa Manyara ipo chini lakini hivi sasa wanafanya jitihada za kuhakikisha yanapungua na watumishi wanapaswa kujitambua afya zao ili waendelee kujitunza ipasavyo. “Hata mimi nimepima ili kuonyesha njia na sisi kama viongozi tunapaswa kufanya hivyo najiamini nipo salama na nivizuri tuwe na utamaduni wa kupima afya zetu kila mara kwa lengo la kujitambua tulivyo,” alisema Maswi.

  Alisema watumishi wa umma wanapaswa kujihadhari na maambukizi mapya ya VVU na kuondokana na athari ya magonjwa sugu yasiyoambukiza kama shinikizo la damu, kisukari, figo, moyo na kupenda kufanya mazoezi.

  “Watumishi wa serikali wanapswa kupima afya zao na kutambua namna walivyo kuliko mtu kuendelea kuishi ili hali hautambui afya yako ipo namna gani na kwa njia hiyo tutatambua nguvu kazi tuliyonayo,” alisema Maswi. Mratibu wa kudhibiti ukimwi wa mkoa huo, Anna Fissoo alisema hali ya maambuki ya VVU kwa mkoa huo siyo kubwa kwani hadi hivi sasa ni asilimia 1.5 ndiyo wana maambukizi huku wilaya ya Simanjiro ikiongoza kwa asilimia 3.2.

  Fissoo alisema maambukizi ya VVU kwa halmashauri ya Babati mjini ni asilimia 2.3, Kiteto ni asilimia 2.2, Babati vijijini ni asilimia 1.7, Hanang’ ni asilimia 1.0 na halmashauri ya wilaya ya Mbulu ina maambukizi kidogo kwa asilimia 0.7
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: WAFANYAKAZI MKOA WA MANYARA WATAKIWA KUPIMA AFYA ZAO MARA KWA MARA. Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top