728x90 AdSpace


 • Habari za hivi Punde

  Tuesday, July 12, 2016

  VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII VYATAKIWA KUBUNI VYANZO VIPYA VYA MAPATO
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw.Enterberth Nyoni(kushoto) akisisitiza jambo wakati wa Kikao Kazi cha Wakuu wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii mjini Dodoma.Katikati ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw. Erasimus Rugarabamu na Mwenyekiti wa Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vilivyo chini ya Wizara hiyo Bw.Paschal Mahinyila.

  Na.Aron Msigwa - DODOMA

  Wito umetolewa kwa Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo Jamii kote nchini kushirikiana na wataalam walio katika vyuo hivyo kubuni vyanzo vipya vya mapato kupitia uanzishaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuviwezesha vyuo hivyo kumudu baadhi ya gharama za uendeshaji zikiwemo za ukarabati wa miundombinu.

  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Enterberth Nyoni ametoa wito huo mjini Dodoma wakati aizungumza na wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vilivyo chini ya wizara hiyo kuhusu namna vinavyoweza kumudu baadhi ya gharama za uendeshaji kupitia miradi mbalimbali.

  "Tuna vyuo vina maeneo makubwa ya wazi ya ardhi ambayo yangeweza kutumika kuongeza kipato kwa shughuli za kilimo na ufugaji, maeneo haya hayatumiki ipasavyo jambo linalosababisha wananchi wayavamie na kuanza kulima jambo ambalo limekuwa chanzo cha migogoro baina ya vyuo husika na wananchi" Amesisitiza Bw. Enterberth.

  Amesema kuwa licha ya vyuo hivyo kubuni miradi kujiongezea kipato, lengo la Serikali ni kuhakikisha inaendelea kuviwezesha vyuo hivyo kwa majengo mapya yanayoendana na hali halisi na hadhi ya vyuo husika ili kwenda na kasi ya mabadiliko ya elimu na mahitaji ya vyuo hivyo.

  Aidha, amefafanua kuwa ipo haja ya kuangalia namna bora ya kuendelea kuiboresha miundombinu ya vyuo vya Maendeleo ya Jamii vilivyopo nchini ili viendelee kuwavutia wanafunzi wanaodahiliwa kusoma katika mazingira bora.

  Amesisitiza kuwa ni vyema vyuo hivyo kuwa na mkakati mkakati wa kujenga majengo mapya ikiwemo madarasa ya kufundishia ili kukidhi mahitaji ya majengo, kuhimili ushindani pia mahitaji ya makundi maalumu.

  Ametoa rai kwa wakuu hao kuangalia upya namna ya kupata fedha nje ya utaratibu wa Bajeti ya Serikali na kuongeza kuwa Serikali itaendelea kuvijengea uwezo vyuo hivyo kulingana na Bajeti inayopangwa ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017 Serikali imetenga shilingi Bilioni 5.6 kwa ajili ya uendeshaji wa vyuo hivyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII VYATAKIWA KUBUNI VYANZO VIPYA VYA MAPATO Rating: 5 Reviewed By: Ahmad Michuzi
  Scroll to Top